BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HAWA NDIYO WANAOTAKA KUTIA MCHANGA KITUMBUA CHA CHUJI, PALE AZAM FC.


Athuman Iddi ‘Chuji’.

AZAM FC leo Jumamosi itahamishia mazoezi yake katika ufukwe wa Coco ambako Yanga pia wapo, lakini kocha wao mkuu Joseph Omog amekiri kupata taarifa zote za rekodi za utovu wa nidhamu za kiungo Athuman Idd ‘Chuji’ lakini hatma yake ni ndani ya wiki moja ijayo.

Chuji yuko katikati kwani inasemekana ameugawa uongozi wa Azam wengine wanamtaka na baadhi hawataki hata kusikia usajili wake. Wanaomtaka wanajenga hoja kwamba apewe mkataba wa miezi sita kuziba nafasi ya majeruhi Frank Domayo lakini kwa masharti mazito huku wanaompinga wakidai kwamba ameshindikana Simba na Yanga sembuse Azam? Kazi ipo.


Omog, alisema amepata taarifa kuwa kiungo huyo ameondolewa katika timu yake ya zamani Yanga kwa matatizo ya nidhamu lakini anataka kujua kila kitu kupitia uchunguzi atakaoufanya ndani ya wiki moja ijayo.


“Nimewapokea nyota wawili wiki hii, mmoja kutoka Haiti (Leonel Saint-Preux) na mwingine kutoka Yanga, lakini huyu wa Yanga nahitaji muda kuweza kujua hatma yake, amefika wiki hii nafikiri mpaka wiki ijayo tutajua nini hatma yake, napata taarifa nyingi juu yake hasa matatizo yake ya nidhamu,”alisema Omog.


“Bado tunaendelea na mazoezi kesho (leo) tutakwenda ufukweni kutafuta pumzi zaidi na wiki ijayo ambayo tutakuwa na mazoezi ya uwanjani nitaweza kufanya uamuzi wa mwisho kwa hawa wachezaji wawili.”


Lakini yeye Chuji mazoezini amekuwa akionyesha ufundi wa aina yake ambao umemfanya kocha Omog raia wa Cameroon kufikiria mara mbili. Kocha huyo alisema amempokea Chuji aliyeomba kujaribiwa katika kikosi chake lakini hawezi kumhakikishia kuwa atamsajili mpaka atakapopata picha kamili ya mwenendo wake.


Chuji alianza mazoezi katikati ya wiki hii Azam FC baada ya kutemwa na Yanga lakini tangu aanze kujifua katika timu hiyo kumekuwa na mgawanyiko kwa viongozi wa juu wa timu hiyo.MWANASPOTI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: