BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ULE UGOMVI WA KUITANA TUMBILI NA MWIZI, WAMFANYA IGP WA TANZANIA KUMWITA MHE DAVID KAFULILA OFISINI KWAKE NA HIKI NDOYO WALICHOTETA..

 
UGOMVI kati ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema, umechukua sura mpya baada ya jana mbunge huyo kuitwa na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu. 


Kafulila na Jaji Werema, walitibuana Juni 25 wakati wa kikao cha Bunge la Bajeti mjini Dodoma, baada ya kurushiana maneno. 



Jaji Werema alipandwa na ghadhabu na kutaka kumtwanga Kafulila baada ya kumwita mwizi, akijibu mapigo ya kuitwa tumbili na mwanasheria huyo mkuu. 





Tafrani hiyo ilitulizwa na baadhi ya mawaziri waliomzuia Jaji Werema asitekeleze azma yake ya kumpiga mbunge huyo. 



Ugomvi huo ulishika kasi Juni 26, baada ya Kafulila kudai kutishiwa maisha na Werema, kwamba kichwa chake kitakuwa halali yake.
Mbunge huyo alifikisha kwa maandishi malalamiko yake ofisi ya spika, akiomba mwongozo wa spika. 



Tanzania Daima jana ilimshuhudia Kafulila majira ya asubuhi akiwasili makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam, yalipo makao makuu ya Jeshi la Polisi nchini.
Alipotafutwa kuelezea kilichompeleka wizarani hapo, alikiri kuitwa na IGP Mangu kuzungumzia suala hilo. 



“Ni kweli nilionana na IGP asubuhi ofisini kwake. Lakini pia nikiwa Dodoma, RCO alichukua maelezo yangu kwa maelekezo ya RPC,” alisema Kafulila na kuongeza: 



“IGP alitaka kujua kuhusu usalama wangu, hivyo nilimweleza… Na alisema ofisi yake inafanyia kazi na itaendelea kufanyia kazi suala hilo la mgogoro huu pamoja na usalama wangu.” 



Kafulila alisema suala hilo bado pia lipo mikononi mwa Katibu wa Bunge na hivyo wao wanasubiri majibu ya Ofisi ya Bunge, ili kama hakuna utata wa kikanuni wamhoji Werema. 



CHANZO CHA UGOMVI BUNGENI.
Siku hiyo, Kafulila aliomba mwongozo kwa Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu kuhusu fedha za akaunti ya Escrow, akidai Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alizungumza uongo mara mbili bungeni kuhusiana na fedha hizo. 



Alibainisha kuwa alisema uongo mbele ya Waziri Mkuu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwamba uamuzi wa kutoa fedha za Escrow kwa IPTL ulikuwa wa mahakama na serikali isingeweza kwenda tofauti. 



Kafulila alibainisha kuwa katika hukumu hiyo ya Septemba mwaka jana, hakuna mstari hata mmoja unaosema kuwa fedha za Escrow wapewe Kampuni ya IPTL. 



Alisema kwamba aliomba mwongozo sababu huo umekuwa mwendelezo wa kuzungumza uongo bungeni. 




Wakati Jaji Werema akijibu mwongozo huo, ndipo alipotumia mifano akiihusisha na mnyama tumbili, kabla ya kumuita mbunge huyo tumbili, hivyo atulie. Kafulila naye akajibu mapigo kwa kumuita mwanasheria huyo mwizi wa fedha za IPTL.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: