Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume
Mtu mmoja anayedaiwa kuwa kinara wa biashara ya madawa ya kulevya kisiwani hapa, amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, akiwa na cocain.
Mtu huyo Sleyum Rashid (39), alitiwa mbaroni na polisi Julai 9, saa 8.45 mchana, akiwa ameficha madawa hayo kwenye mikoba 14 ya kike.
Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Yussuf Ilembo alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa mara baada ya kushuka katika ndege ya Shirika la Oman Na. WY. 717 iliyokuwa ikitokea Muscat.
Alisema mtuhumiwa alikamatwa na kupekuliwa katika sanduku lake aliloingiza mizigo yake na kukutwa mikoba 14 ya kike na kila mmoja ukiwa na dawa za kulevya iliyoshonewa kwa ndani ya mikoba hiyo ikiwa na uzito wa kilo 5.605.
“Mtuhumiwa alikuwa akitumia hati ya kusafiria yenye namba AB 363906 iliyotolewa Desemba 29, 2009 na makao makuu ya uhamiaji jijini Dar es Salaam,” alisema Ilembo.
Alisema kwa mujibu wa hati yake, mtuhumiwa amekuwa akisafiri nchi mbalimbali ikiwemo Brazil, China, Japan, Hong kong, Afrika Kusini na nchi za Kiarabu.
Alisema polisi pia limewashikilia wafanyakazi wanne wa uwanja wa ndege ambao walikuwa na mahusiano na mtuhumiwa huyo.
Ilembo alisema wakati wa kulindana, kuoneana aibu sasa umekwisha hivyo kila mmoja anawajibu wa kulilinda taifa.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment