SARAFU YA SH 500 KUZIBA PENGO LA NOTI YA SH 500 ILIYOSHINDWA KUHIMILI KWA WANANCHI.
Mfano wa Sarafu ya 500 kama iliyoonekana katika Banda la Benki Kuu katika maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Noti ya shilingi mia tano.
Baada ya noti ya shilingi mia tano kubainika kuwa kwenye mzunguko mkubwa sana na hivyo kuchakaa mapema, Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeamua kuleta sarafu ya shilingi mia tano mwaka huu wa fedha inayotegemewa kudumu kwa miaka zaidi ya ishirini.
Sarafu ya shilingi mia tano inatarajiwa kuzinduliwa na Benki Kuu ya Tanzania katika siku za usoni. Sarafu hiyo itatumika sambamba na noti za shilingi mia tano huku zikiwa zinaondolewa kwenye mzunguko taratibu taratibu. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki na Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania, Emanuel Boaz.
0 comments:
Post a Comment