UJERUMANI, UFARANSA ZAWAFUNGISHA VIRAGO NIGERIA NA ALGERIA KATIKA HATUA YA 16 BORA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014.
Nigeria jana ilishindwa kutimiza ndoto ya kuungana na Senegal, Cameroon na Ghana kuwa moja ya timu za Afrika zilizowahi kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia baada kukubali kipigo cha 2-0 kutoka kwa Ufaransa.
Algeria nayo ilikumbana na wakati mgumu baada na wenyewe kulala mbele ya Ujerumani kwa kupokea kipigo cha bao 2-0 kwenye mchezo wa raundi ya 16 bora.
0 comments:
Post a Comment