BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATU 17 WA FAMILIA MOJA WAPOTEZA MAISHA KATIKA MJI WA GAZA.


Makombora ya Israel yalipua majumba katika eneo la Gaza.
 
Maafisa wa Palestina wanasema kuwa watu kumi na saba wa familia moja wameuawa baada ya makombora ya Israel kuharibu nyumba moja ya ghorofa tatu ya mkuu wa polisi wa Hamas.

Tayseer Al-Batsh anadaiwa kujeruhiwa katika shambulizi hilo.

Mashambulizi hayo yanajiri baada ya wapiganaji wa Hamas kurusha makombora ya masafa marefu katika miji ya Israel ikiwemo Tel Aviv.

Maafisa wa Israel wanasema kuwa makombora mawili ya Roketi yalirushwa kutoka lebanon lakini yakaanguka katika eneo lililo wazi kazkazini mwa Israeli.

Na katika hatua ya kulipiza kisasi ,Israel ilirusha makombora nchini Lebanon na kuzidisha hofu kwamba huenda mzozo huo ukapanuka.

Takriban raia 150 wa Palestina wameuawa katika mashambulizi hayo huku ikiwa hakuna vifo vyovyote vilivyoripotiwa nchini Israel.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: