Watumishi wa wa sekta binafsi na serikalini wameanza kuwekewa mikakati ya kuboresha maisha na asasi isiyo ya kiserikali ya maendeleo ya wanawake Tanzania ya Inuka yenye lengo la kuwapunguzia makali ya maisha katika mkoa wa Morogoro.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa Mratibu wa asasi isiyo ya kiserikali ya maendeleo ya wanawake Tanzania (INUKA), David Msuya alisema kuwa asasi hiyo imeanza kuboresha maisha ya watumishi wa wa sekta binafsi na serikalini kwa kutoa mikopo ya riba nafuu.
Msuya alisema kuwa asasi hiyo ilifanya utafiti wa kina na kubaini kuwa wananchi wengi wamekuwa na hofu ya kuchukua mikopo katika taasisi za fedha kutokana kuwepo kwa masharti magumu.
Inuka ilianza kutoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo wadogo na sasa wameelekeza mkakati wa kuwakopesha watumishi wa serikali na binafsi kuanzia shilingi mil.25 alisema Msuya.
“Lengo la utekelezaji wa mpango huo wa kuboresha makazi ya watumishi ni moja ya hatua ya kusaidiana na serikali katika kupunguza kero na makali ya maisha kwa wananchi hususan watumishi wa serikali ambao licha ya kuwa ni sehemu ya jamii lakini mishahara wanayopata hakidhi mahitaji halisi ya ukali wa maisha.”Aalisem Msuya.
Msuya aliongeza kwa kusema kuwa asasi hiyo kabla ya kutoa mkopo mwa mtumishi hupewa elimu ya ujasiriamali pamoja na mfumo rasmi wa matumizi ya fedha kabla ya kukabidhiwa ili malengo walijiwekea kwa mujibu wa mkataba yaweze kuleta tija kwa taifa.
Mbali na mikakati hiyo changamoto wanazokumbana nazo kutoka kwa wateja wao baadhi yao sio waaminifu pindi wanapopata mikopo hushindwa kurejesha kwa wakati na wengine hutomokea kabisa jambo ambalo linarudisha nyuma malengo ya asasi hiyo katika kuwahudia wananchi kwa wingi zaidi.alisema Msuya.
Asasi hiyo katika mkoa wa Morogoro imeweza kuwahudia wananchi 200 kutoka Morogoro mjini, Gairo, Kilombero ambapo jumla ya shilingi mil.24 zilitumika kuwakopesha wajasiriamali wadogowadogo ili kuwaongezea mitaji yao.
0 comments:
Post a Comment