BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKE WA RAIS JAKAYA KIKWETE AFICHUA SIRI ZA WATOTO WA KIKE TANZANIA KUFANYA NGONO MAPEMA.

 
Mtoto akiwa amejifunika majani usono, Picha ya mtandao.
 
WATOTO wa kike nchini wametajwa kujihusisha katika mapenzi katika umri mdogo kuliko wa kiume.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete alisema takwimu zinaonesha kwamba asilimia 13 ya wasichana, wanaanza kufanya mapenzi wakiwa na umri wa chini ya miaka 15 wakati kwa upande wa wavulana ni asilimia saba.
Alisema hayo wakati akifungua Mkutano uliojadili Elimu ya Afya ya Uzazi na Jinsia kwa Vijana, ulioandaliwa na Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Gerd Mueller na kufanyika katika ofisi za Ubalozi wa nchi hiyo mjini New York, Marekani.

Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama), pia alisema zaidi ya wasichana milioni 58 duniani, wameolewa wakiwa na umri wa chini ya miaka 18, miongoni mwao wakiwemo wa miaka 10.

Alisema kitendo hicho, kinachangia wengi wao kupata maambukizi ya Ukimwi na wengine kufanyiwa ukatili wa kijinsia.

Alisema kitendo cha wasichana, kujihusisha na mapenzi wakiwa na umri mdogo, kinafanya wakabiliwe na tatizo la mimba za utotoni na hivyo wengi wao kushindwa kupata elimu.

“Nchini Tanzania kati ya msichana mmoja hadi wanne wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 19 wana mimba au watoto , takwimu hizi ni kubwa zaidi katika nchi zingine za Ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kusini,” alisema Mama Kikwete.

Kwa mujibu wake, idadi hiyo inaonesha wasichana wataendelea kuwa kundi lililoathirika kwa kukosa haki zao za kupata afya, watakabiliwa na unyanyasaji na maisha yao yataisha mapema.

Alisema vijana wa Afrika, wanatakiwa kupewa elimu ya maisha, afya ya uzazi na usawa wa jinsia, ambayo itaendana na mila na desturi zao wawe na uchaguzi mzuri wa maisha yao. Mueller alisema zaidi ya miaka 20, Serikali yake imekuwa ikifanya kazi ya kuhakikisha vifo vya wajawazito na watoto, vinapungua na upatikanaji wa huduma ya uzazi wa mpango inaimarika.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: