MEYA WA JIJI LA LONDON AIKUBALI TANZANIA.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Soko la Mitaji (CMSA), Fatma Simba na Meya wa Jiji la London, Fiona Wolf wakipongezana baada kutia saini makubaliano ya ushirikiano kati ya CMSA na Taasisi ya Usalama na Uwekezaji ya Uingereza (CISI) jijini Dar es Salaam juzi. Picha na Emmanuel Herman.
Dar es Salaam. Meya wa Jiji la London, Fiona Woolf amesema Tanzania ina nafasi nzuri ya kunufaika na uwekezaji kutokana na kuwepo kwa mazingira yanayovutia wawekezaji katika sekta zote muhimu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika ziara yake ya kwanza jana, meya huyo alisema hiyo ni moja ya sababu zilizomfanya kufanya ziara na kundi la wafanyabiashara kutoka katika jiji la London kwa ajili ya kuangalia maeneo muhimu ya uwekezaji na kuangalia namna ya kushiriki katika kujenga mitaji.
Woolf pia alitia saini makubaliano maalumu baina ya Mamlaka ya Soko la Mitaji (CMSA) na Taasisi ya Taaluma ya Usalama na uwekezaji (CISI) cha Uingereza kwa ajili ya kusaidia kujenga uwezo wa kitaaluma katika masuala ma masoko ya mitaji.
“Hiki ni kutu cha kipekee kabisa kwa ajili ya kuendeleza ushirikiano katika kujenga uwezo wa kitaaluma hasa kwa kubadilishana uzoefu baina ya Uingereza na Tanzania. Inasaidia kuboresha taaluma na kusaidia katika ujenzi wa mazingira bora zaidi kwa siku zijazo,” alisema.
Alisema kuna fursa nyingi sana za uwekezaji kwa Tanzania ndiyo sababu iliyomsukuma kuleta ujumbe wa wafanyabiashara nchini, pia kufanya mazungumzo na baadhi ya wafanyabiashara wa ndani kwa ajili ya kujenga ushirikiano baina yao.
Awali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa CMSA, Fatma Simba alisema kutiwa saini makubaliano hayo ni sehemu muhimu katika kuinua taaluma ya soko la mitani na kuingiza ujuzi wa kimataifa nchini. Alisema CMSA inajivunia kiuazna ushirikiano huo na CISI ambacho ni chombo inachoheshimika zaidi kimataifa katika kusimamia taaluma ya masoko ya mitaji duniani.
“Ushirikiano huu utasaidia soko la mitaji nchini kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwa na wanataaluma wenye ushindani wa kimataifa kutokana na mafunzo watakayopata katika makubaliano haya,” alisema.
Alieleza kwamba makubaliano hayo pia yatakuwa na manufaa makubwa katika kukuza utaalamu wa utoaji huduma katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya nchi za Kusini mwa Afrika (Sadc) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment