Na Mtanda Blog.
Septemba 14/2014.
Klabu ya Polisi Moro SC imewatambulisha wachezaji wake wapya kwa kicheko baada ya kuisambatisha Burkina FC katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na ligi kuu ya vodacom Tanzania bara katika msimu wa mwaka 2014/2015 kwa ushindi mnono wa bao 4-1 uliofanyika uwanja wa jamhuri Morogoro.
Mshambuliaji Edger Edger alifungua kalamu ya mabao kwa kupachika bao la kwanza dakika ya 12 huku dakika ya 35 Nicolaus Kabipe akifunga la pili na mshambuliaji mpya Danny Mrwanda alikamilisha bao la tatu katika dakika ya 45 na kwenda mapumziki wakiwa na bao tatu.
Kipindi cha pili Polisi Moro waliendeleza mashambulizi langoni mwa Burkina FC na dakika ya 62 Mula Majuto aliongeza huku bao la kufutia machozi la Burkina lilifungwa katika dakika ya 42 na mshambuliaji Victor Mswaki.
Mwamuzi wa mchezo huo Seleman Kinugani alimzawadia kadi nyekundu kiungo mshambuliaji Saidi Manga kwa kumchezea vibaya mchezaji wa Polisi Morogo.
0 comments:
Post a Comment