UKUBWA DAWA !!!. MIZENGO PINDA AOKOA JAHAZI KWA KUIOKOA MAHAKAMA YA KADHI.
Dodoma. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana alilazimika kuokoa jahazi la ‘kuzama’ kwa Katiba Mpya kwa kupoza hasira za Waislamu kuhusu Mahakama ya Kadhi kutoingizwa kwenye Katiba inayopendekezwa.
Badala yake Pinda aliwaahidi kuwa Januari mwakani, Serikali itawasilisha bungeni muswada wa sheria ili kuutambua uamuzi unayofanywa na Mahakama za Kiislamu.
Tamko hilo lilitokana na kuwapo kwa hali tete bungeni juzi na jana baada ya Waislamu kuhamasishana kupiga kura ya Hapana iwapo Mahakama hiyo isingeingizwa kwenye Katiba.
Wakati wajumbe Waislamu wakishikilia msimamo huo, baadhi ya wajumbe dini nyingine waliweka msimamo kupiga kura ya Hapana kama ibara hiyo ingeingizwa kwenye Katiba. Hali hiyo iliisukuma Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalumu chini ya Mwenyekiti, Samuel Sitta kukutana mfululizo na baadhi ya viongozi wa dini na Waziri Mkuu kwa ajili ya kutafuta mwafaka.
Akitoa tamko la Serikali, Pinda aliahidi kuwa Januari mwakani, Sheria ya Mahakimu sura ya 11 na Sheria ya Kiislamu sura ya 375 zitafanyiwa marekebisho ili kutambua uamuzi wa Mahakama ya Kadhi. Lengo ni kuhakikisha umoja na mshikamano vinadumu kwa Watanzania, ikiwamo kuyakubali maeneo saba yanayolalamikiwa na Waislamu. Alisema wajumbe katika kamati ya uongozi walijiridhisha kuwa madai ya Waislamu kuhusu Kadhi ni ya msingi.
Pinda alisema kutokana na hotuba hiyo ya Waziri wa Katiba na Sheria, Ofisi ya Waziri Mkuu ililibeba suala hilo na kuunda jopo kwa ajili ya kulishughulikia.
Sheikh Hamid Masoud Jongo, alisema wajumbe na Waislamu wamemsikia (Pinda) jinsi alivyojifunga kuhusiana na kutambulika kwa hukumu za Mahakama ya Kadhi.Askofu Donald Mtetemela alisema Mahakama ya Kadhi imekuwa ikileta hofu kwa Waislamu na Wakristo.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment