BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

EBOLA YASABABISHA MWANDISHI WA HABARI WA MAREKANI ASHTAKIWE NA MAAFISA WA WA UTAWALA LIBERIA


Maafisa wa utwaala nchini Liberia, wanasema kuwa watamshitaki mwanamume aliyepatikana na ugonjwa wa Ebola nchini Marekani wakimtuhumu kuwa alitoa taarifa za uongo kuhusu kukutana na jamaa wake aliyekuwa anaugua ugonjwa huo. Wasafiri wanakaguliwa na kuulizwa maswali kabla ya kusafiri kutoka Liberia

Mgonjwa huyo Thomas Eric Duncan alitakiwa kujibu maswali kadhaa kabla ya kusafiri kwenda Marekani mwezi jana lakini maafisa wanasema aliulizwa ikiwa alikutana na jamaa yake mwenye virusi hiyo akasema la. Alisema hakuna jamaa yake yeyote anaugua ugonjwa huo.

Lakini waziri wa afya amesema kuwa mwanamume huyo alionekana akimpeleka jamaa wake mgonjwa hospitalini. Liberia ni moja ya nchi zenye idadi kubwa ya wagonjwa wa Ebola katika kanda ya Afrika Magharibi

Bwana Duncan yuko katika hali mahututi, katika hospitali ya Dallas.

Ni mgonjwa wa kwanza wa Ebola kugudnulika nchini Marekani ambako zaidi ya watu 100 wanachunguzwa ikiwa wameambukizwa ugonjwa huo. Ni maafisa wa afya pekee wanaoruhusiwa kuwachukua wagonjwa kutoka majumbani kwao

Zaidi ya watu 3,330 wamefariki kutokana na Ebola katika nchi nne za kanda ya Afrika Magharibi.

Taarifa ya kutaka kumfungulia mashitaka mghonjwa huyo ilitolewa katika mkutano wa kila wiki wa serikali kuarifu waandishi wa habari kuhusu hali ya ugonjwa huo nchini humo.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: