BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS KENYATTA AKAMBIDHI MADARAKA WILLIAM ROTO KUONGOZA KENYA KWA MUDA WAKATI AKIENDA KATIKA MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA ICC


Kenyatta amemkabidhi mamlaka kwa muda naibu wake William Ruto kwa siku mbili atakazokuwa nje.

Mahakama ya kimataifa ya ICC, inajianda kuwa mwenyeji wa mkutano maalum wa siku mbili kuhusu kesi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye atakuwa rais wa kwanza aliye mamlakani kufika mbele ya mahakama hiyo. 

Kenyatta anakabiliwa na tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu anazodaiwa kutenda baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.


Mahakama hiyo inasama kuwa Kenyatta alihusia katika kupanga na kufadhili ghasia za kikabila baada ya uchaguzi uliozua utata mwaka 2007/08 Zaidi ya wakenya 1,000 waliuawa kwenye gasia hizo. Ruto ambaye ni rais kwa muda naye pia anakabiliwa na kesi katika mahakama hiyo ya ICC.

Mawakili wa Kenyatta wanasema kuwa kesi hiyo inapaswa kufutiliwa mbali kwa kukosa ushahidi.


Kenyatta ameombwa na mahakama hiyo kufika mbele yake ili kujadili malalamiko yaliyowasilishwa na kiongozi wa mashtaka Fatou Bensouda kwamba serikali ya Kenya imekataa kuwasilisha ushahidi unaohitajika katika kesi ya Kenyatta. 


Majaji wa mahakama hiyo hata hivyo watathmini kauli kutoka kwa pande zote mbili.


Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa pia kutangaza tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi ya Kenyatta. 


ICC imemtaka Kenyatta kujibu madai ya upande wa mashitaka kuwa Kenya inakataa kutoa ushahidi unaotakikana na mahakama hiyo.

Rais Kenyatta akikagua gwaride la heshima kabla ya kuondoka nchini kuelekea Hague.

Mwezi Septemba, mahakama iliahirisha kesi dhidi ya Kenyatta baada ya upande wa mashitaka kusema kuwa Kenya imekosa kutoa ushahidi unaotakikana na mahakama hiyo.


Mashahidi wa upande wa mashitaka wamejiondoa katika kesi hiyo.
Mamia ya wabunge wa Kenya wanatarajiwa kuambatana na Kenyatta kama ishara ya kumuunga mkono.CHANZO BBC SWAHILI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: