Mshambuliaji wa kimataifa kutoka Uganda Emmanuel Okwi ameendeleza furaha katika klabu yake ya Simba sc baada ya kufunga bao muhimu dhidi ya Mtibwa Sugar uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Polisi Moro sc chini ya Kocha msaidizi John Tamba aliambulia kipigo kutoka kwa JKT Ruvu kwa bao 1-0, shukrani za pekee kwa nahodha wa kbalu hiyo Mohamed Faki aliyefunga bao kwa adhabu ndogo baada ya walinzi wa Polisi Kufanya madhambi eneo la hatari.
Kocha mkuu wa klabu ya Polisi Moro Mohamed Adolph Rishard aliachishwa kazi kwa matokeo mabaya hali iliyopelekea kocha msaidizi kushika kwa muda mikoba yake.
Stend United ilikiona cha choto mbele ya Prison FC jijini Mbeya baada ya kuchapwa bao 3-1 katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati Ruvu Shooting Stars iliibana mbavu Coastal Union kwa kutoka sare ya bao -1-1.
0 comments:
Post a Comment