Katibu mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro juzi. Juma Mtanda.
Juma Mtanda, Morogoro.
Katibu mkuu wa chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) Dk Wilbroad Slaa ameeleza kuwa Tanzani kwa sasa inasifika nje ya nchi kwa utawala wa udikteta chini ya rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro juzi, Dk Slaa alisema kuwa ndani ya miaka mitano Tanzania imeingia katika sifa ya utawala wa kidikteta kutokana na kuvunjwa kwa haki nyingi za binadamu.
Dk Slaa alisema kuwa ushahidi upo wazi kwa Tanzania kuingia katika nchi zinazokiuka haki za binadamu hasa kwa kushindwa kufuata misingi ya utawala bora na badala yake imekuwa ikivunja haki za binadamu.
“Wananchi tuelewe kuwa hili halina ubishi, kwa Tanzania kuingia katika orodha za nchi zinazotawala kwa udikteta chini ya utawala wa rais Kikwete, kuna matukio mengi ya uvunjari wa haki za binadamu kwa watu kuuawa na vitendo vingine.”alisema Dk Slaa.
Aliongeza kwa kusema kuwa hivi karibuni yeye alikuwa nje ya nchi (Marekani) kwa ziara maalumu lakini wakati akiwa huko aliongea na waandishi wa habari katika kituo kimoja cha redio na kati ya mambo aliyoulizwa ni juu ya utawala bora kwa nchi ya Tanzania lakini kuna wakati alilazimika kujibu maswali hayo kwa moyo wa uzalendo.
“Kuna mambo mengine katika maswali ililazimika nijibu kwa uzalendo lakini nilishushuliwa kwa kuelezwa kuwa Tanzania ndani ya miaka mitano nyuma imekuwa ikiongoza nchi kwa udikteta na imengia katika rekodi za nchi zinazoongoza kwa udikteta chini ya rais Kikwete.”alisema Dk Slaa.
Dk alisema kuwa hilo ni kweli kwani utawala wa rais Kikwete umeingia katika sifa hiyo kutokana na kukiukwa kwa kiasi kikubwa haki za binadamu na mifano ipo wazi kwa viongozi wa dini kufanyiwa mambo ya ukatili ndani ya magereza.
Hili jamani nalisema lakini sina Kiswahili kizuri zaidi ya kusema kuwa viongozi wa dini wamekuwa wakilawitiwa magerezani jambo ambalo si kitendo kizuri kwani viongozi hawa wamekuwa wakiheshimika ndani ya jamii.alisema Dk Slaa katika mkutano huo.
Kuna idadi ya viongozi 51 wa dini ambao wamekamatwa na vyombo vya dola kutokana na makosa mbalimbali lakini viongozi hao baadhi yao wamejikuta wakifanyiwa mambo ya kulawitiwa katika magereza.
Mimi nawaheshimu sana tu viongozi wa dini inakuwaje kiongozi anafanya kosa Zanzibar alafu anakuja kushtakiwa mahakama ya Tanzania bara .?alihoji Dk Slaa.
Kwa upande mungine Dk Slaa ameitaka serikali kuboresha mishahara ya watumishi wake ili kuondokana na vitendo vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watumishi katika idara mbalimbali.
Hali sio nzuri kwa watumishi wa serikali kutokana na kukithiri kwa vitendo vya rushwa na kudai kwaa sasa rushwa imevuka mipaka hasa ndani ya jeshi la polisi.
“Tumesikia baadhi ya vituo vya polisi hivi karibuni kuvamiwa lakini ni nani anavamia vituo vya polisi kwa lengo gani.?”alihoji Dk Slaa.
Dk Slaa alisema kuwa kuvamiwa kwa vituo vya polisi kunasababishwa na askari polisi na kumtaka mkuu wa jeshi la polisi nchini kutoendekeza kukaa ofisini na badala yake kwenda katika vituo kujua matatizo yanayowakabili watumishi wake.
Dk Slaa alisema kuwa (yeye) amekuwa akipata taarifa nyingi kutoka kada mbalimbali za uozo wa utendaji kazi ndani ya serikali na taasisi zake na kufahamu mambo mengi yanayoshindwa kutatuliwa na viongozi husika.
“Kuna tukio limefanywa na askari polisi la kukamata watu waliokuwa wakisafirisha nyara za serikali lakini waliwaachia baada ya watu hao kutoa kitu kidogo na kuwaachia lakini wakawaarifu wenzao ili wawakamate ili nao wawapatie kitu kidogo.”alisema Dk Slaa.
Aliongeza kwa kusema kuwa mchezo huo ulifanywa na askari wa awali lakini baada ya kuwaachi waliwasiliana na wenzao wa kituo kinachofuatiwa nao wakawamata na kutaka wapewe fedha ili wawaachie.
Dk Slaa alidai kuwa baada ya wahalifu hao kushindwa kutoa fedha walizotaka askari wa pili, walikubaliana kuliacha gari kituo cha polisi ili wakafuate fedha wawalipe wawaachie waendelee na safari yao.
Wahalifu wale waliporudi tena kituoni hapo walifyatua risasi na kuwajeruhi askari kabla ya kupora silaha na kuondoka na gari lao ambalo lilikuwa na nyara za serikali.
Akizungumzia suala la kuchakachuliwa kwa katiba mpya chini ya Jaji Joseph Walioba, Dk Slaa alisema kuwa suluhisho la kuulinda muungano baada ya maoni ya wananchi ni kuwepo kwa serikali tatu ikiwemo ya Tanganyika, Muungano na Zanzibar.
Dk Slaa alisema kuwa kama serikali itang’ang’ania na katiba iliyochakachuliwa basi, wapinzani wapo tayari kampeni za uchaguzi mkuu wa oktoba 2015 kuingiza ajenda ya kuwashawishi wananchi kupata katiba mpya 2016.CHANZO/MTANDA BLOG
0 comments:
Post a Comment