BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KLABU YA POLISI MORO SC YAPIGA HESABU KALI KUBAKI LIGI KUU TANZANIA BARA.


Kocha mkuu kwa sasa wa klabu ya Polisi Moro sc, John Tamba kulia akiwa na wachezaji wake muda mfupi kabla ya kuanza mchezo baina yao na Ndanda FC ambapo katika mchezo huo Polisi Moro SC waliibuka na ushindi wa bao 2-0 katika uwanja wa jamhuri Morogoro.

Na Juma Mtanda.
 Klabu ya Polisi Moro SC ipo katika hesabu kali za kukwepa mstari wa kushika daraja baada ya kufanya vibaya katika ligi kuu Tanzania bara.


Akizungumza mjini hapa na Mtanda Blog, Kocha Mkuu wa klabu ya Polisi Moro SC kwa sasa, John Tamba alisema kuwa kwa sasa klabu hiyo ipo katika mahesabu ya kukwepa kushuka daraja na kitu kilichopo mbele yao ni kushinda michezo zote iliyobakia.

Tamba alisema kuwa hakuna kitu wanachofikiria zaidi ya kuinusuru timu hiyo isishuke daraja na ili kukwepa janga hilo wameweka mikakati ya kushinda michezo yao mitatu ili wakae katika msimamo mzuri utaosaidia kukwepa mstali wa kushika daraja baada ya ligi kumalizika.


Polisi Moro SC inakibarua kigumu kukwepa janga hilo kwani jumatano (kesho) itashuka dimba la uwanja wa jamhuri Morogoro kuwania pointi tatu muhimu mbele ya Coastal Union kabla ya kuwavaa vinara wanaongoza ligi hiyo Yanga SC April 27 katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.


“Hesabu zetu zinaanza kwanza na timu ya Coastal Union ya Tanga kesho (jumatano) na lengo letu ni kuibuka na ushindi na baada ya hapo hesabu zitaahamia kwa Yanga SC April 27 kisha tunamaliza na Mbeya City Mei 02 kwani baada ya hapo hesabu zitakuwa zimekamilika kujua kama tutabaki ligi kuu ama laa.


Msemaji wa klabu ya Polisi Moro SC, Mwanaidi Lwena akizungumzia msimamo wa klabu hiyo alisema kuwa wana kazi ngumu na mzito ya kuhakikisha timu inabakia ligi kuu msimu ujao kwani mpaka sasa wana pointi 24 baada ya kucheza michezo 23.

Lwena alisema kuwa kazi kubwa iliyopo mbele yao ni kufanya vizuri kwa michezo iliyosalia lakini kazi hiyo ya ushindi itaanza kushinda mchezo wao dhidi ya Coastal Union yenye pointi 27.


“Mchezo wetu na Coastal Union kesho ni kama fainali kwetu kwani tunahitaji kushinda kupata pointi tatu zituvushe kufikia pointi 27 huku tukiomba kuzifunga Mbeya City na Yanga ili kujinusuri na janga la kushuka daraja”.alisema Lwena.


Lwena alisema kuwa kwa sasa timu hiyo ipo chini ya kocha John Tamba ambaye ni kocha mkuu baada ya Amri Saidi aliyepewa mikoba ya Mohamed Rishard Adolph kutokuwepo katika timu hiyo.


Timu kwa sasa ipo chini ya kocha John Tamba kama kocha mkuu kwani Amri Saidi aliyerithi mikoba ya Mohamed Adolph Rishard kuondoka klabuni.


Lwena alisema Amri Saidi aliaga kama ana matatizo na hajarudi mpaka leo na hizi mechi zilizosalia hawana haja ya kusaka kocha mkuu mungine.


Vinara wa ligi hiyo Yanga SC wanaongoza ligi kwa kukusanya pointi 49 baada ya kuongeza pointi muhimbi mbele ya Stend United kwa ushindi wa bao 3-2 huku Azam FC ikiwa imejiwekea kibindoni pointi 41 wakati Simba SC ikiwa na pointi 35 na Prison ikiburuza mkia kwa pointi 22.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: