Mkazi wa mtaa wa Kilongo kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro, Asha Mohamed (27) amenusurika kupigwa na wananchi wenye hasira baada ya kudaiwa yeye na mume wake kumtesa mtoto wao kwa kumfunga kamba kwa masaa 15 kisha kumfungia ndani ya nyumba mkoani hapa.
Akizungumza na mwandishi wa Mtanda Blog katika eneo la tukio Mwenyekiti wa mtaa Kilongo B kata ya Mkundi mkoani hapa, Leila Victor Chuma alisema kuwa ililazimika kupoza hasira za wananchi waliozingira nyumba ya, Asha Mohamed wakitaka kumdhuru baada ya kufichuka kwa kitendo cha ukatili cha kumfungia ndani ya nyumba mtoto wao huku akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi na kulazwa kifudifudi.
Chuma alisema walipata taarifa za kuwepo kwa kitendo hicho asubuhi ya juzi
“Nilipata taarifa za kuteswa kwa mwanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi Kilongo kwa kufungwa kamba mikononi na miguuni asubuhi ya leo (jana) kisha kufungiwa mlango na kofuli ndani ya nyumba ili asitoke ikiwa sehemu ya adhabu ya kuunguza chandarua.”alisema Chumba.
Mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Asha Mohamed ambaye amenusurika kipigo alisema kuwa tukio hilo wakati linafanyia yeye hakuwa akilitambua na amekuja kulitambua baada ya kutoka soko la Mawenzi alikokwenda kununua bidhaa kwa ajili ya kuweka katika genge.
“Ninachoweza kusema hili tukio la kufungwa kamba kwa mwanangu nimekuja kulijua baada ya kuambiwa na mwanaye mwinginw kuwa kaka yake Salum Mohamed amefungwa kamba na baba yake.”alisema Asha.
Aliongeza kwa kusema kuwa anachofahamu mtoto wake wa kiume Salum Mohamed amefanya kosa la kuchoma chandarua usiku wa jana (juzi) kwa madai ya chandarua hiyo imechakaa na haifai kutumia.
“Lengo la mtoto wetu baada ya kumhoji alieleza kuwa amechoma moto chandarua hiyo kutokana na kuchakaa imekuwa ndogo hivyo njia sahihi ya kununuliwa mpya ameona bora aichome ili apatiwe itayokidhi mahitaji.”alisema Asha.
Kutokana na tukio hilo, askari wa jeshi la polisi walifika eneo hilo na kuamuru kuvunjwa kwa kofuri la mlango ili kuokoa maisha ya mtoto huyo aliyekutwa amelala kifudifudi kwa masaa 15 huku akiwa amefungwa kamba.
Mtanda Blog hili lilishuhudia mtoto huyo akiwa amelala kifudifudi katika godoro huku mikono na miguu ikiwa imekutanishwa kwa kufungwa kwa kamba hali iliyomfanya ashindwe kulala vizuri.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alipotafutwa kwa njia ya simu alisema kuwa jeshi la polisi linawashikiria wazazi wa mwanafunzi kwa tuhuma za kumfunga kamba mtoto huyo.
0 comments:
Post a Comment