BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WANAJESHI WA SERIKALI WATIMUA MBIO KUWAKIMBIA WANAMGAMBO WA ISLAMIC STATE MJI WA RAMADI.

http://www.dw.de/image/0,,17341492_303,00.jpgMaelfu ya raia wa Iraq wanaendelea kuukimbia mji wa Ramadi huku kundi la wanamgambo wa Islamic State likiwazuia na kuendeleza mashambulizi ya kuudhibiti mji wa Ramadi.

Waasi hao wameuteka mji huo kutoka kwa vikosi vya serikali.

Umoja wa mataifa unasema kuwa watu elfu 25 wameutoroka mji huo katika siku kadhaa zilizopita, wakielekea mashariki hadi mjini Baghdad.

Raia wapatao elfu mia moja na thelathini walitoroka mji huo mwezi uliopita, ulipovamiwa na kundi la Islamic State.

Shirika la umoja wa mataifa pamoja na mashirika mengine, yameanza kusambaza chakula, maji na dawa, huku pia kambi za muda zikijengwa.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: