BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WANANCHI WALIOTOROKA GHASIA ZA KUMPINGA RAIS NKURUNZIZA ASIGOMBEE URAIS NCHINI BURUNDI KWA USAFIRI WA MASHUA, 15 WAFARIKI DUNIA TANZANIA.



Wakimbizi 15 wa Burundi, wamefariki kutokana na ugonjwa wa kipindupindu, baada ya kukimbilia usalama wao nchini Tanzania kwa mashua wakitokea nchini mwao Burundi.


Hayo ni kwa mujibu wa mashirika ya utoaji misaada.

Inasemekana kuwa wengine kadhaa wanaugua ugonjwa huo.

Shirika la Oxfam, linasema kuwa zaidi ya wakimbizi elfu sabini kutoka Burundi, wamefika katika rasi moja kisiwani nchini Tanzania, baada ya kutoroka ghasia za kisiasa nchini Burundi.

Kwa sasa wanahamishwa kwa mashua kutoka kisiwani humo, hadi nchi kavu.

Kuna upungufu mkubwa wa maji safi ya kunywa, chakula, makaazi na huduma za kimatibabu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: