BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ASKARI POLISI NA MAJAMBAZI WARUSHIANA RISASI ENEO LA CLOCK TOWER JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

Name:  Exim 1.jpg
Views: 7856
Size:  180.9 KBKuna taarifa inayoeleza kuwa watu wanaodaiwa kuwa na silaha wamekamatwa eneo la benki ya Exim clock Tower baada ya kurushiana risasi na askari polisi huku baadhi yao  wakifanikiwa kukamatwa Jijini Dar es Salaam leo.

 
Taarifa hiyo imeeleza kuwa majambazi hayo hawakuiba benki hiyo ya Exim isipokuwa walikuwa wanafuatiliwa na polisi wakiwa katika gari aina ya Noah kutoka Posta na walipofika mzunguko wa magari wa Clock Tower wakaanza kurushiana risasi.

Baadhi ya majambazi wametiwa nguvuni na askari polisi wakiwemo watatu waliokuwa wanatumia gari aina ya toyota Spacio. Chanzo:Jamiii Forums




Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: