BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KAZI INAPOKUWA NGUMU !! RAIS KIKWETE HUWA ANAHAHA KUSAKA USHAURI.

http://mobile.mwananchi.co.tz/image/view/-/2727800/medRes/1018919/-/5v5bx/-/jk+dodoma.jpg?format=xhtml

Dodoma. Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete alilazimika kutafuta ushauri kutoka kwa watu mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha kazi ya mchujo wa wagombea urais kuisha salama, chama hicho kilisema jana.



Kikao cha Kamati Kuu, ambacho ratiba ya awali ilionyesha kingefanyika Julai 9, hakikuweza kufanyika kama ilivyopangwa na badala yake kilifanyika jana jioni mpaka usiku, hali iliyosababisha vikao vingine kuchelewa kuanza pia.


Akizungumza na waandishi wa habari jana, katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema mwenyekiti huyo alikuwa akitafuta ushauri kwa watu mbalimbali na ndio maana vikao hivyo vya juu havikuweza kufanyika katika muda uliopangwa.


Nape alisema sababu nyingine ya kuchelewa kwa vikao hivyo ni shughuli za chama na Serikali alizokuwa akizifanya Rais Kikwete, ambaye juzi alizindua ukumbi mpya wa chama hicho na baadaye mchana alihutubia Bunge kwa ajili ya kulivunja.


“Mwenyekiti alikuwa na vikao mbalimbali vya consultation (mashauriano) na wadau ili kuhakikisha vikao vinakwenda salama,” alisema Nape.


Hata hivyo, Nape hakuelezea vikao vya mashauriano kati ya Rais Kikwete na Serikali vilihusisha makundi gani.


Lakini Rais Kikwete kwa mujibu wa Katiba ni Amiri Jeshi Mkuu na pia ndiye mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Taifa inayohusisha majeshi yote na wadau wengine.


Hata hivyo, kumekuwa na minong’ono mingi kwamba baadhi ya kambi za wagombea wenye nguvu na ushawishi zilikuwa zikiendelea na vikao usiku kucha kwa ajili ya kuweka mikakati ya jinsi ya kufanikisha azma za wagombea wao.


Licha ya kambi hizo pia kumekuwa na makundi ya wapambe wa wagombea waliojazana katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma, kwa kila kundi kutambia kundi jingine kwamba lazima washinde kwa namna yoyote, hali iliyoonekana kuashiria uwezekano wa kutokea uvunjaji wa amani.


Polisi wamekuwa wakifanya doria kwenye maeneo yenye baa kwa ajili ya kuwalazimisha wamiliki kufunga sehemu hizo za biashara kwa mujibu wa muda uliowekwa kisheria.


Kwa mujibu wa ratiba ya awali iliyotangazwa na Nnauye, Kamati ya Maadili na Usalama ya Taifa ilikuwa ifanyike Julai 8 na kufuatiwa na Kikao cha Kamati Kuu (CC) Julai 9 na kisha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa jana na kufuatiwa na mkutano mkuu leo na kesho.


Kutokana na sababu hizo, Nnauye alisema Kamati ya Maadili na Usalama na CC vingefanyika jana kabla ya NEC kukutana leo na kuendelea na Mkutano Mkuu.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: