Zanzibar. Baraza la Mitihani nchini Necta leo limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha sita na kusema kuwa umefaulu umeongezeka kwa asilimia 0.61.
Akitangaza matokeo hayo mjini Zanzibar leo, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde alisema mwaka huu idadi ya ufaulu ni asilimia 98.87 ikilinganishwa na asilimia 98.26.
Dk Msonde alisema jumla ya watahiniwa 38,853 wamefaulu mitihani hiyo kati ya watahiniwa 40,753 waliofanya mitihani hiyo ya kumaliza kidato cha sita. Aliongeza kuwa kuna watahiniwa 35 ambao walishindwa kufanya mitihani yao baada ya kuugua ghafla. Dk Msonde aliongeza kuwa kati ya waliofaulu, wasichana ni 11,734 na wavulana ni 27,119.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment