BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MGOMBEA URAIS WA CCM Dk JOHN MAGUFULI: ACHIMBA MKWARA MAPEMA NA KUELEZA KUWA HATAOGOPA MTU.



Mgombea mteule wa urais kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, Dk John Magufuli ametambulishwa rasmi leo katika viwanja vya Zakhiem, Mbagala jijini Dar es Salaam.



Akizungumza katika viwanja hivyo, Magufuli alisema iwapo atapata ridhaa ya kuongoza nchi atahakikisha haki inatendeka kwa Watanzania wote. 


“Nataka niseme kwa dhati sitawaangusha, nitafanya kazi kweli kweli, sitamuogopa mtu na wala sitapenda mtu wa chini aonewe,” alisema Dk Magufuli.


Aliongeza kuwa atahakikisha anasimamia Ilani ya CCM na kuitekeleza. Magufuli aliwashukuru Watanzania kwa sala zao kwani katika mchakato mzima alikuwa akiwasihi wamuombee.


“Kupitishwa kwangu inadhihirisha wazi mlikuwa mnaniombea na sala zenu zimesikilizwa na mwenyezi Mungu #UkaribishoWaMagufuli,” alisema.mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: