BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAUMINI 27 WAFARIKI DUNIA KUTOKANA NA MKANYAGANO WAKATI WA SHEREHE ZA KIDINI ZA MAHA PUSHKARALU.

 
Zaidi ya mahujaji 27 wameuawa kufuatia mkurupuko uliotokea katika warsha moja ya kidini katika jimbo la Andhra Pradesh nchini India.

Mkanyagano huo ulitokea wakati wa kuanza kwa sherehe za Maha Pushkaralu ambapo maelfu ya watu waliokuwa wamekusanyika kuoga kwenye maji ya mto Godavari walianza kusukumana.

Mkurupuko huo ulitokea mwendo wa saa nane u nusu katika mji wa Rajahmundry

Polisi wanasema kuwa umati ulikimbia kwenda kwa lango la kuinga mtoni.

Mikurupuko kama hii hutokea kwa wingi wakati wa warsha za kidini nchini India ambapo watu wengi hung'ang'ania nafasi katika maeneo madogo.
Waandalizi wanasema kuwa takriban watu milioni 24 wanatarajia kushiriki katika hafla hiyo inayotarajiwa kudumu kwa siku 12.

Mahujaji hao wa dini hiyo wanaamini kuwa kuoga na maji ya mto huo huosha mtu madhambi yake.

Waziri mkuu wa jimbo hilo Andhra Pradesh bwana Chandrababu Naidu, alisema kuwa inahuzunisha mno kuwa mahujaji waliokuwa wakitarajia kuosha madhambi yao wanaangamia.

Mwaka wa 2013 watu 115 walipoteza maisha yao katika mkurupuko uliotokea katika hafla ya kidini ya wahindu katika jimbo la Madhya Pradesh.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: