
Alisema Waziri wa Ujenzi ambaye atamteua, anapaswa kufanyakazi kubwa ambayo itamzidi yeye na kuahidi kukamilisha miradi mbalimbaliya barabara kwa kiwango cha lami na kuzindua miradi mipya.
Dkt. Magufuli aliyasema hayo jana katika Wilaya ya Mpanda, mkoani Katavi ikiwa ni siku moja baada ya CCM kuzindua kampeni zake katika Viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam.
Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza, Dkt. Magufuli alisema anatambua kero mbalimbali walizonazo ikiwemo ya ukosefu wa miundombinu ya barabara, zahanati, maji na nyinginezo.
Aliongeza kuwa, kero hizo atazitatua kwa wakati baada ya kuingia Ikuluna kuunda Baraza la Mawaziri ambalo litafanyakazi kwa viwango.
"Mkoa wenu una tatizo kubwa la miundombinu ya barabara, nitajengakutoka Mpanda hadi Uvinza-Kigoma ya kilomita 194 kwa kiwango cha lami, tayari upembuzi umefanyika, ujenzi unaanza 2016.
"Mimi ndio Magufuli, nawaomba Oktoba 25, mwaka huu, hakikisheni mnachagua CCM tuweze kutekeleza haya ninayowaahidi," alisema na kuongeza kuwa, mbali ya kujenga barabara ya Mpanda hadi Uvinza,pia atajenga barabara inayotoka Mshamu hadi Tongwe Ziwani.
Dkt. Magufuli aliwahakikishia wananchi waishio mpakani waliokuwawakimbizi na kupatiwa uraia wa Tanzania, kuondoa shaka kwani tayarini Watanzania hivyo waishi kwa amani bila presha.
"Serikali ya CCM itahakikisha mnaishi kwa amani kama walivyo Watanzania wengine na mtapata haki zote, kinachotakiwa ni kuichagua CCM Oktoba 25, mwaka huu, "alisema
Alisema mbali ya kujenga barabara, pia ataimarisha sekta ya afya na kuongeza ujenzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo vya elimu ya juukatika mikoa mbalimbali na kuhakikisha tatizo la maji linabaki historia.
Awali akimkaribisha Dkt. Magufuli, Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, aliwataka wananchi mkoani humo kumchagua mgombea urais wa CCM kwani hakuna chama kingine kinaweza kuwaletea maendeleo.
Aliwataka wananchi wawachague wagombea wa CCM kuanzia urais,wabunge na madiwani ili waweze kuwaletea maendeleo. Chama hicho kimezindua kampeni zake juzi na hivi sasa, Dkt. Magufuli na mgombeamwenza, Bi. Samia Suluhu Hassan wameanza kuzunguka mikoani.MAJIRA
0 comments:
Post a Comment