BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KOCHA MKUU WA KLABU YA RUVU JKT STARS AMWAGIA SIFA MSHAMBULIAJI MPYA KWA KUPACHIKA MABAO.

 
Mshambuliaji mpya wa klabu ya JKT Ruvu Stars, Gaudence Mwaikimba.

Na Juma Mtanda, Morogoro.
KOCHA Mkuu wa kikosi cha JKT Ruvu Stars, Felix Minziro amemwagia sifa mshambuliaji mpya Gaudence Mwaikimba na kueleza kuwa usajili wake utaleta manufaa baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kupachika mabao katika michezo ya kirafiki.

Akizungumza na gazeti hili mjini Morogoro ambako wameweka kambi ya kujiandaa na ligi kuu Tanzania bara msimu wa mwaka 2015/2016, Minziro alisema kuwa mshambuliaji huyo aliyetokea Azam FC atatisha katika klabu yake kwa kufumania nyavu za wapinzani wake.

Mwaikimba atashirikiana vyema na mshambuliaji mwenzake Saidi Kipanga na wengine kuhakikisha timu hiyo inaibuka na ushindi kutokana na ushirikiano wao.

Minziro alisema kuwa ujio wa Mwaikimba tayari umeonyesha kuimarisha safu ya ushambuliaji na jambo hilo ndilo linolotakiwa na benchi la ufundi, mashabiki na wadau wa soka wa klabu hiyo.

“JKT Ruvu imelamba dume kwa usajili wa Gaudence Mwakimba na tuna amini benchi letu la ufundi ndoana yake ya usajili imenasa kifaa muhimu.”alisema Minziro.

Minziro alisema kuwa mchezaji huyo ameonyesha uwezo mkubwa wa kufunga katika mechi zao nne za kirafiki kwa kupachika mabao ya kiufundi.

Katika mchezo wa kwanza wa kujipima nguvu dhidi ya JWTZ Combaine na JKT Ruvu waliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Mwaikimba kabla ya kufunga bao lingine moja katika ushindi wa bao 3-2 dhidi ya Lipuli ya Iringa katika michezo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Minziro ameeleza kuwa katika michezo y kirafiki iliyofanyika mkoani Morogoro, Mwaikimba ameweza kufunga bao katika mchezo na Mtibwa Sugar katika ushindi wa bao 1-0 huku akipachika bao tatu katika ushindi wa bao 4-2 mbele ya Polisi Moro SC katika michezo iliyofanyika uwanja wa jamhuri Morogoro.

Timu ya JKT Ruvu imeweka kambi ya kujiandaa na ligi kuu Tanzania bara mkoani Morogoro huku ikifanya mazoezi yake katika uwanja wa shule ya sekondari ya Morogoro.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: