BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI NAMNA ALIVYOPELEKWA MAHABUSU YA SEGEREA JIJINI DAR ES SALAAM.


Lawrent Masha akitoka Mahakama ya Kisutu baada ya kesi yake kusikilizwa leo. Picha na Said Hamis

Dar es salaam.
Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa shitaka la kutoa lugha ya matusi kwa maofisa wa polisi hapo jana.

Baada ya kusomewa shitaka hilo, Masha amekana na kurudishwa Segerea hadi hapo nyaraka zake zilizowasilishwa kwa ajili ya dhamana zitakapohakikiwa.

Masha amefikishwa mahakamani hapo akiwa na vijana wengine 19 ambao wamesomewa shitaka la kutaka kukusanyika bila kibali.

Awali taarifa zinasema Masha alifika katika Kituo cha Polisi cha Osterbay jijini Dar es Salaam jana jioni kwa lengo la kutaka kuwadhamini vijana hao na baadaye alishikiliwa na polisi kituoni hapo.

Masha alikihama Chama cha Mapinduzi hivi karibuni na kujiunga na Chadema na kuteuliwa kugombea Ubunge katika Jimbo la Sengerema katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba.

Mashitaka yanayomkabili waziri huyo wa zamani yanatarajiwa kusomwa baadaye leo mchana.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: