BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KIPINDUPINDU CHAUA WATU 17 NA 2,000 KUKUMBWA NA UGONJWA HUO TANGU KUANZA AGOSTI 17 MWAKA HUU KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM PEKEE.

 Mmoja wa wakimbizi kutoka nchi jirani akiwa anapata matibabu ya ugonjwa wa kipindupindu katika kambi ya Nyarugusu Tanzania.
 
Dar es Salaam. Idadi ya watu waliopoteza maisha kwa ugonjwa wa kipindupindu imeongezeka na kufikia 17 baada ya watu wengine wawili kupoteza maisha jana.


Hata hivyo, idadi ya watu walioripotiwa kuugua ugonjwa huo tangu ulipuke katika Jiji la Dar es Salaam Agosti 17, imefikia 2,000.

Ofisa Habari wa Manispaa ya Temeke, Joyce Msumba alisema kuwa jana walipokea wagonjwa wapya saba na kati yao, mmoja ameshafariki dunia.

Msumba alisema wagonjwa wengi hawatoki katika Manispaa hiyo bali wapo wanaotoka eneo la Buguruni katika Manispaa ya Ilala na Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Alisema tayari wameshatoa taarifa kwa maofisa wa afya wa wilaya zao ili wafuatilie hali katika familia zao.

Watoto wakicheza katika jalala eneo la Bugando Mwanza, mazingira ya namna hii ni hatari kwa afya zao. 

 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Victorina Ludovick alisema wamepokea wagonjwa wapya 31 idadi inayofanya watu waliolazwa katika kambi ya ugonjwa huo kufikia 38.

Dk Ludovick alisema wagonjwa wengi wanatoka maeneo ya Buguruni, Vingunguti, Jangwani, Ilala, Mchikichini, Tabata na Kigogo.

Alisema kuendelea kusambaa kwa ugonjwa huo kunatokana na wakazi wengi wa maeneo hayo kutozingatia kanuni za afya wanazofundishwa na wataalamu.

“Magari ya matangazo yanapita katika mitaa yao kila siku kutoa elimu na kuwahamasisha kunawa mikono kwa sabuni baada ya kutoka chooni, kuchemsha maji ya kunywa na kuzingatia usafi wanapoandaa vyakula,” alisema Ludovick

Alisema maofisa afya wanaendelea na kazi ya kukagua mazingira wanayofanyia kazi wafanyabiashara wa vyakula na matunda ili kuwabaini wanaokiuka agizo la kuacha kufanya biashara hiyo hadi ugonjwa huo utakapokwisha.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: