Hayo yamesemwa leo katika mwendelezo wa mpango wa kusikiliza kero za wananchi kuhusu maswala ya ardhi kwa upande wa wakazi wa Ilala na Temeke jijini Dar es Salaam ambapo jana zilisikilizwa kero 153 za wakazi wa Kinondoni.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Dk. William Lukuvi amesema katika Manispaa ya Kinondoni tatizo kubwa linalosabababisha kero za ardhi ni uvamizi wa maeneo ya wazi na viwanja vya watu pamoja na kuvunjiwa nyumba zao na watu wanaodaiwa kuwa matapeli. Jumla ya watu 28 wamelalamikia tatizo hilo.
Pia amewapa tahadhari matapeli wanaofanyanyia wananchi wanyonge na masikini na kudhani kwamba serikali haipo makini kuangalia kinachoendelea “watashughulikiwa na hata kama halitaisha kwa siku moja.”
Amesema, jumla ya kero 112 zimepokelewa na na kufikia idadi ya 265 kaunzia jana kwa wananchi wa wilaya zote tatu za Dar es Salaam.
Lukuvi amesisitiza kuwa, atahakikisha kila mwananchi aliyewasilisha kero yake kuhusu ucheleweshaji wa hati za umiliki wa ardhi na nyumba kabla ya Octoba 25.
0 comments:
Post a Comment