Tarehe 23 mwezi wa kwanza mwaka 2014 mafariko yalibomoa daraja la Magole barabara kuu ya Dodoma-Morogoro na kusababisha miundombinu ya barabara kushindwa kupitika kwa siku takribani siku nne, Picha anaonekana Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli (mwenye kofia ya pama) akisimamia kazi za ujenzi wa barabara hiyo inarejea kwa haraka na magari yaweze kupita.
Magari baada ya tatizo hilo yalikuwa yakilazimika kuzunguka kupitia barabara ya Iringa-Morogoro kwa kupita njia panda ya Melela-Kilosa, Kimamba kisha kutokea Dumila ambapo adha hiyo ilikuwa ikiwakumba wasafari wa wanaoelekea mikoa ya Mwanza, Kagera na nchi jiraza na wale waliokuwa wakielekea Morogoro na Dar es Salaam wakifuata mfumo huo.
Haya ni baadhi ya matukio yaliyokuwa yamejitokea wakati wa kuhakikisha ujenzi wa barabara unarejea kwa haraka.
Dk Magufuli ni mmoja wa wagombea urais kupitia chama cha mapinduzi huku akikabiliana na upinzani mkali kutoka kwa waziri aliyejiuzulu Edward Lowassa naye akigombea urais kupitia Ukawa katika uchaguzi mkuu unaoratajia kufanyika Oktoba 25 mwaka na wagombea wengine wa ngazi hiyo wakiwemo na nafasi ya ubunge na udiwani.
0 comments:
Post a Comment