BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KAULI YA KUKOSEA MANENO YA RAIS JAKAYA KIKWETE KWAZUA HOFU JUU YA IDADI KAMILI YA WAPIGAKURA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 25.


Rais Jakaya Kikwete, akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Kiongozi wa Mbio za Mwenge, Juma Khatib Chum katika sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge zilizofanyika Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma jana. Picha na Freddy Maro

Dar es Salaam.
Kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa jana na kukosea idadi ya wapigakura kwenye kituo maalumu cha huduma kwa wateja cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). walioandikishwa kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu, imeongeza idadi ya wananchi waliopiga simu

Akiwa kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Julius Nyerere, aliyekuwa rais wa kwanza wa Tanzania, yaliyofanyika kitaifa mjini Dodoma Rais Kikwete alisema idadi ya wapigakura wanaostahili kwa Tanzania Bara ni milioni 28 na visiwani ni zaidi ya laki tano.

Kauli hiyo inakinzana na idadi iliyotangazwa na NEC mapema wiki hii ambayo ni milioni 22.75 hivyo kuzua sintofahamu miongoni mwa wananchi juu ya idadi halisi ya Watanzania watakaoshiriki uchaguzi hapo Oktoba 25. Ingawa baadaye Ikulu ilirekebisha kauli hiyo kupitia vyombo vya habari, wadau walitaka ufafanuzi kutoka NEC.

Mkuu wa Kitengo cha Habari NECo, Clarence Nanyaro amelieleza gazeti la Mwananchi kuwa kituo hicho kimezidiwa na idadi ya simu zinazoingia kiasi cha kupoteza ufanisi wake wa kutoa huduma inayostahili hivyo kuhitaji matengenezo madogo.

“Mwitikio umekuwa mkubwa sana kuliko ilivyotazamiwa. Tangu uzinduzi ulipofanyika leo saa 5:00 asubuhi simu 2,400 zilipokelewa. Na jana, mpaka saa 7:00 zilizopokelewa ni 3,010. Mashine imepoteza uwezo wake na tunafanya jitihada za kuirekebisha ili iendelee na kazi.

Miongoni mwa simu nyingi zinazopokelewa ni zile zinazotaka ufafanuzi juu ya kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa jana. Tunaendelea kuwaelimisha wananchi kwamba idadi kamili ni ile iliyotangazwa na tume na si vinginevyo.”

Hata hivyo tume imewataka wananchi kuendelea kupiga namba 0800 782 100 ili kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusiana na uchaguzi mkuu lakini wanaweza kutoa taarifa juu ya jambo linalokiuka maadili au kuvunja sheria za nchi kuelekea siku ya uchaguzi.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: