BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KIHONDA STAR YAIBUKA BINGWA KOMBE LA KUHAMASISHA WATU KUPIGA KURA OKTOBA 25 MOROGORO.

Afisa Michezo Manispaa ya Morogoro, Asteria Mwang'ombe na Katibu Mkuu wa chama cha soka wilaya hiyo, Kafale Maharagande wakisalimiana na wachezaji wa timu ya Kihonda Star wakati wa michezo ya kombe la Kuhamasisha watu kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura Oktoba 25 iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Jitegemee kata ya Chamwino Manispaa ya Morogoro.PICHA/Juma Mtanda


Na Juma Mtanda

Timu ya soka ya Kihonda Star FC imetwaa ubingwa wa kombe la Kuhamasisha watu kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura katika uchaguzi mkuu Oktoba 25 na kukabidhiwa zawadi ya sh150,000 baada ya kuikung’uta Msamvu City bao 6-5 katika mchezo mkali wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msimgi Jitegemee kata ya Chamwino Manispaa ya Morogoro.

Mashindano hayo yenye kauli mbiu ya “vijana tumia haki yako ya kidemokrasia kuchagua kiongozi bora 2015 kwa kuzingatia misingi ya amani” ilishirikisha timu nne kutoka kata nne za Chamwino ikiwa na timu ya Chamwino Rangers FC, Mwere Academy ya Nunge, Kionda Stars kutoka Kihonda na Msamvu City kata ya Mwembesongo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo mjini hapa, Katibu wa chama cha soka wilaya ya Morogoro (MMFA), Kafare Maharagande alisema kuwa mabingwa hao wamekabidhiwa zawadi ya sh150,000 baada ya kuilaza Msamvu City kwa bao 6-5 zilizopatikana kwa njia ya changamoto ya mikwaju ya penalti baada ya kumalizika dakika 90 bila kufunga na mshindi kuamuliwa kwa njia hiyo.

Maharagande alisema kuwa mashindo hayo yalianzia hatua ya nusu fainali na fainali ya kwanza Msamvu City iliambulia kipigo cha bao 7-6 kutoka kwa Kihinda Star baada ya sare ya bao 1-1 wakati fainali ya pili Mwere Academy nayo ikiisambaratisha Chamwino Rangers kwa bao 3-0.

“Kihonda Star imefanikiwa kuibuka mabingwa wa mashindano ya Kuhamasisha watu kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura Oktoba 25 kwa kuilaza Mwere Academy FC kwa penalti 6-5 baada ya dakika 90 kumalizika bila kufungana katika mchezo huo wa fainali na kukabidhiwa zawadi ya mshindi wa kwanza ya sh150,000.”alisema Maharagande.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa kwa pamoja na taasisi ya Restless Devolopment Initiative Tanzania na Morogoro Youth Devolopment (Moyodei) zimekuwa zikitoa elimu ya uraia, michezo ya sanaa na ubunifu, usawa wa kijinsia na ujasiliamali.

Mwezeshaji wa kitaifa wa shirika la Restless Devolopment Tazania, Salu Charles alisema kuwa malengo ya mashindano hayo yamefanikiwa kwa kiwango kikubwa hasa baada ya vijana kujitokeza kwa uwingi wakati wa michezo hiyo.

Akitaja zawadi za washindi katika michezo hiyo, Charles alisema kuwa mshindi wa kwanza amekabidhiwa zawadi ya sh150,000 huku mshindi wa pili timu ya Mwere Academy FC wakiondoka na kitita cha sh80,000 wakati wa tatu Msamvu City ikipata kiasi cha sh60,000 na Chamwingo Rangers ikiambulia kiasi cha sh50,000.MTANDA BLOG
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: