BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VIONGOZI WA KANISA WAKWIBA FEDHA ZA SADAKA.


Mahakama nchini Singapore imewapata na hatia ya ufisadi, viongozi sita wa kanisa kongwe na kubwa zaidi nchini humo.

Muasisi wa kanisa la City Harvest, Kong Hee na watu wengine watano wanadaiwa kuwa waliiba dola milioni 17 hazina ya kanisa.

Yamkini Hee na washirika wake walikuwa wakizitumia pesa hizo kwa harakati zake zilizoshindwa za kumfanya mkewe kuwa nyota wa kimataifa wa nyimbo chapa Pop.

Dola zingine milioni 19 zilitumika kuficha kile walichofanya.
Viongozi hao wa kanisa hilo wanadai kuwa muziki ulikuwa njia mojawepo ya kuwafikia watu wasio wakristo, lakini mahakama ilikatalia mbali wazo hilo.

Sasa viongozi hao wamo katika hatari ya kufungwa jela maisha.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: