BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MGOMBEA WA URAIS WA CCM AAHIDI KUMWAGA NEEMA KWA WAKULIMA WA ZAO LA KOROSHA MIKOA YA KUSINI

 

MGOMBEA urais wa CCM, Dk John Magufuli amesema akichaguliwa kushika nafasi hiyo, atatumia utajiri wa gesi uliopo katika mikoa ya Kusini, kutoa ruzuku kwa vifaa vya ujenzi ili kushusha bei na kuwawezesha wananchi kujenga nyumba bora.

Amesema pia atatumia nafasi hiyo kutafuta namna bora ya kuwainua wakulima wa korosho, tofauti na utaratibu wa sasa wa stakabadhi ghalani, aliosema umekuwa ukiwasababishia umasikini mkubwa wakulima wa zao hilo.

Katika hatua nyingine, mgombea huyo amesema mgombea ubungewa CCM katika Jimbo la Mtama, Nape Nnauye anawindwa usiku na mchana, ikiwa nipamoja na kuwekewa mikakati asichaguliwe kutokana na jitihada zake za kupambanana ufisadi na wizi wa mali ya umma.

Aliyasema hayo alipohutubia wakazi wa miji ya Nachingwea, Ruangwa, Mtama na ziara yake hiyo ya kampeni kwa Mkoa wa Lindi, iliyohitimishwa kwa mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Mpilipili mjini Lindi.
Mgombea urais kupitia CCM, Dk John Magufuli akihutubia wakazi wa Lindi mjini kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mpilipili jana. Habari Uk.8 (Picha na Adam Mzee).
Mgombea urais kupitia CCM, Dk John Magufuli akihutubia wakazi wa Lindi mjini kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mpilipili jana. Habari Uk.8 (Picha na Adam Mzee). 

Akiwa Nachingwea, Ruangwa, Mtama na Lindi Mjini, DkMagufuli alisema tofauti na wapinzani wanaoahidi kuondoa nyumba za nyasi na tembe nchinzima kwa siku 100 watakazokaa Ikulu, jambo alilosema ni ndoto, Serikali yake itakachofanya ni kushusha bei ya mabati, saruji, nondo, misumali na vifaa vingine vya ujenzi ili wananchi wajenge nyumba bora.

Akielezea ni vipi atawezesha hilo kufanikiwa, Dk Magufuli alisema atatumia utajiri wa rasilimali za Taifa ikiwemo gesi inayopatikanakatika Mikoa ya Kusini na Bagamoyo, Pwani ili kutoa ruzuku katika vifaa vya ujenzi.

Lakini, pia kuongeza viwanda vya bidhaa hizo ili kushusha bei kwa kiwango cha juu. Alisema dalili za kushuka kwa vifaa hivyo, zimeanza kuonekana baada ya kujengwa kwa Kiwanda cha Saruji cha Dangote mkoani Mtwara, ambachokinatumia nishati ya gesi kwa uzalishaji, kilichowezesha kushuka kwa bei ya saruji kutoka Sh 16,000 hadi Sh 8,000 na kwamba bei hiyo itashuka zaidi atakapokuwa rais.

Alisema pia ataziba mianya yote ya rushwa serikalini ili makusanyo ya fedha hizo yatumike kuboresha maisha ya Watanzania wakiwemo wa Kusini, huku akisema ushahidi wa utendaji wake kwa watu wa Kusini ni ujenzi wa barabara za lami kutoka Dar es Salaam kwenda Lindi na Mtwara na baadaye Tunduru na Songea.

Ili kumwezesha kuingia Ikulu, mgombea huyo aliwaomba wakaziwa Mkoa wa Lindi kufika katika vituo vya kupiga kura mapema asubuhi ya Oktoba25, huku akisema kutokana na vitisho na vurugu zilizopangwa ili kuwatishia wananchi hasa wanawake wasipige kura, kutakuwa na polisi wa kutosha ili kulinda amani.

Akizungumzia soko la korosho, Dk Magufuli alisema akiingiaIkulu atabadili mfumo wa ununuzi wa korosho ili kuwezesha wakulima wa zao hilo kwa mikoa ya Kusini, kunufaika na kuboresha maisha yao na kuachana na mfumo wasasa ambao unawafanya wakulima kukopwa fedha zao bila kulipwa na hivyo kuwamasikini.

“Jamani mimi Shahada yangu ni ya utafiti wa korosho, naifahamu korosho kuanzia chini hadi juu. Nafahamu thamani ya zao hilo kwa kila sehemu yake na hata hilo ganda mnalolitupa ni fedha, naomba mnichague nijeni waboreshee kilimo cha korosho na maisha yenu,” alisema Dk Magufuli.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: