BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA WA TANZANIA AFARIKI DUNIA WAKATI AKIPATIWA MATIBABU NCHINI INDIA


Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Handeni Tanga na Waziri wa Viwanda na Biashara, marehemu Abdalah Kigoda.


Dar es salaam.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Handeni Tanga na Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdalah Kigoda amefariki dunia jana nchini India alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Taarifa iliyotolewa jana na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Ofisi ya Bunge zinasema kuwa, Waziri Kigoda amefariki majira ya saa kumi jioni katika Hospitali ya Appolo nchini India.

Taarifa hizo zimeeleza kuwa kuhusu taratibu za msiba huo, ikiwa ni pamoja na kuusafirisha mwili wa marehemu na mipango yote ya mazishi zitaendelea kutolewa na Serikali pamoja na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu kadri zitakavyoendelea kupatikana. 


Waziri huyo alipelekwa India kwa matibabu mapema mwezi Septemba.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: