BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

PENGINE MCHUNGAJI CHRISTOPHER MTIKILA ALIWAHI MNO KUZALIWA KATIKA NCHI YA TANZANIA !.

 
NIKIWA kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Pugu kati ya mwaka 1992 na1994, nilikuwa miongoni mwa wanafunzi ambao kila Jumamosi ilikuwa lazima twende Mnazi Mmoja, katikati ya Jiji la Dar es Salaam. 

Ilikuwa tunakaa huko siku nzima hadi jioni tukishindia mihogo ya kuchoma iliyokuwa inauzwa na vijana pembeni mwa barabara. Safari yote hiyo tulikuwa tunaenda kumsikiliza Mchungaji Christopher Mtikila aliyekuwa akitoa mihadhara ya bure na katika mazingira yasiyo rasmi. 

Mihadhara yake ilikuwa ni mikali ikihusu Uhuru wa Tanganyika na jinsi nchi yetu ilivyokuwa ikiporwa na watu aliowaita magabachori. Alieleza kwa ufasaha sana kuhusu historia ya Uhuru wa Tanganyika na jinsi nchi yetu ilivyojaliwa utajiri wa rasilimali nyingi ambazo kama isingekuwa magabacholi nchi yetu ingekuwa paradiso. Kwa uzito wa hoja zake na umahiri wa kuzielezea ilikuwa ni vigumu mno kuacha kumsikiliza bila kuchoka, ama moja kwa moja au kupitia katika sauti iliyorekodiwa katika kaseti. 

Alikuwa na mvuto na nguvu kubwa ya kuongea bila kuchoka. Tungeweza kukaa Mnazi Mmoja tukimsikiliza tangu saa tano asubuhi hadi saa kumi jioni na kurudi zetu shuleni Pugu. Baada ya Mnazi Mmoja tulihamia Jangwani ambapo Mtikila alikuwa akijaza watu wakisikiliza hotuba zake za saa ya ukombozi. Wakati huo ndio mwanasiasa pekee aliyekuwa na uwezo wa kuitisha maandamano na vijana wakamfuata Jangwani. 

Tulilundikana na tukaandamana mitaa ya Jangwani tukielekea Mnazi Mmoja bila kujua hasa tunaenda wapi hadi tulipotawanywa kwa mabomu ya machozi ya polisi. Tungesambaratika na sisi wanafunzi tungerudi zetu shuleni, na jioni nzima hiyo tungekaa kujadiliana hoja za Mtikila. Alitujaza upepo vizuri sana na tukaamini kabisa kwamba matatizo ya nchi hii ilikuwa ni hao magabachori. 

Nakumbuka katika mkutano mmoja Jangwani alijenga hoja na akawatia watu hasira dhidi ya magabachori. Tukiwa hapo, ndege ilipita angani na kwa hasira watu walianza kurusha mawe kuelekea angani wakiamini kwamba ndege hiyo ilikuwa imewabeba magabachori! 

Nilipojiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1995 niliendelea kumfuatilia Mchungaji Mtikila. Wakati huo alikuwa akija pia kutoa mihadhara katika ukumbi maarufu wa Nkrumah. Kama kawaida yake, alikuwa anajaza ukumbi, siku aliyokuja chuoni wanafunzi wasingefanya chochote zaidi ya kumsikiliza. 

Kabla ya Augustine Mrema kuhamia NCCR-Mageuzi mwaka 1994/1995, Mtikila ndiye aliyekuwa mwanasiasa machachari wa upinzani aliyekuwa na uwezo wa kuitisha maandamano wakati wowote na watu wakamfuata. Umaarufu wake uliyumba baada ya kuanza kumpinga Mrema, wakati huo Mrema akiwa lulu na mtu yeyote aliyempinga Mrema alionekana ametumwa au kununuliwa na CCM. 

Hali hii tunaiona tena mwaka huu, na hivi karibuni kabla ya kifo chake Mtikila aliingia matatizoni kwa kumpinga vikali mwanasiasa ‘lulu’ kwa sasa na ambaye baadhi ya vyama vya upinzani vimewaaminisha wananchi kwamba ndiyo mwarobani wa mabadiliko na matatizo yote hapa nchini. 

Namkumbuka pia Mchungaji Mtikila kama mwanasiasa pekee aliyekuwa na ujasiri wa kumkosoa Nyerere waziwazi bila woga na watu wakamsikiliza. Aprili 28, mwaka 1998 nikiwa Rais wa Chama cha Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) niliitisha maandamano ya wanafunzi kuelekea Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu. Maandamano hayo, pamoja na mengine, yalikuwa na lengo la kuishinikiza serikali iongeze bajeti ya elimu. 

Hata hivyo maandamano hayo hayakufika mwisho kwani yalisambaratishwa kwa mabomu ya machozi Ubungo. Siku mbili baada ya maandamano hayo, Mchungaji Mtikila aliniita nyumbani kwake wakati huo akiwa anakaa katika ‘flats’ za NHC maeneo ya Kariako, karibu na Kiwanda cha TBL. Niliwakuta akiwa yeye na mke wake. 

Aliniambia kuwa “wana mpango wa kukufukuza chuo kwa sababu ya kuitisha mgomo wa wanafunzi. Lakini usiwe na wasiwasi tumeshakutafutia chuo huko Zimbabwe. Kwa hiyo endelea na harakati za ukombozi”. 

Sikutilia maanani maneno ya Mchungaji Mtikila na nilirudi zangu chuoni nikaendelea na shughuli za masomo na urais wangu wa DARUSO. Hata hivyo, Mei 13 mwaka huo wa 1998 nilipokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu. 

Barua hiyo ilinitaarifu nia ya serikali ya kunifutia udhamini wa masomo yangu kwa kuitisha mgomo wa wanafunzi. Ndipo nikakumbuka maneno ya Mtikila. Niliijibu barua hiyo na nikatoa taarifa kwa wanafunzi na baada ya hapo hakuna kilichofuata hadi nilipomaliza masomo yangu mwaka 1999. 

Nilitambua kwamba Mchungaji Mtikila alikuwa na taarifa za ndani sana hadi hata akajua kwamba ningefukuzwa chuo kabla ya taarifa hizo kunifikia rasmi. 

Lakini pia katika mazungumzo yake ni mtu ambaye alikuwa na taarifa za ndani mno za Tanzania na dunia kwa ujumla na ilikuwa ni vigumu kujua chanzo chake cha taarifa, hasa ukizingatia kwamba ilikuwa ni vigumu kujua kiwango rasmi cha elimu ya mwanasiasa huyu. Nimeendelea kumfuatilia Mchungaji Mtikila katika harakati zake nyingi. 

Ni mwanasiasa ambaye amekuwa akipanda na kushuka na kupanda tena katika ulingo wa kisiasa nchini, lakini ni mwanasiasa ambaye alikataa kabisa kupotea katika ulingo wa siasa hadi mauti inamkuta. Binafsi nitamkumbuka Mtikila kwa mambo makubwa matatu. Mosi, ni uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja na umahiri wa lugha za Kiswahili na Kiingereza. 

Nakumbuka mwaka 1998 alipokuja Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanafunzi walitaka azungumze kwa Kiingereza wakiamini kwamba haimudu hiyo lugha, na wakati huo Kiingereza mlimani kilikuwa kinathaminiwa sana kama sio kuabudiwa. 

Mtikila aliongea kwa Kiingereza fasaha mno hadi wote tukabaki midomo wazi. Pili, Mtikila alikuwa ni mwanasiasa aliyeamini katika kusema kweli bila kujali ukweli huo ungemuudhi au kumfurahisha nani. 

Kwa kifupi yeye alikataa kuwa mnafiki. Jambo hili lilimuingiza matatizoni mara kwa mara kutokana na mazingira yetu ya siasa ambapo uwongo, ulaghai na ubabaishaji katika siasa ni sifa ya kuwa mwanasiasa. Tatu, ambalo linaendana na hili la pili, ni kwamba Mtikila alikuwa king’ang’anizi wa misingi aliyoaiamni. 

Kwa mfano, yeye tangu mwanzo kabisa wa harakati za kudai mfumo wa vyama vingi aliamini kuwepo kwa Katiba Mpya itakayotambua na kurejesha hadhi ya Tanganyika kama nchi. Wanasiasa wengi wamekuwa wakiyumba katika hili jambo la katiba mpya lakini yeye alibaki na msimamo huo hadi anafariki. 

Yeye aliamini mapema kabisa uwepo wa mgombea binafsi hadi akapigania haki hiyo mahakamani. Mtikila alishinda kesi kuhusu haki ya mgombea binafsi mara tatu, mbili katika Mahakama za Tanzania mwaka 1993 na 2005, na moja katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu mwaka 2010. 

Mambo haya matatu yanamfanya Mtikila kuwa mwanasiasa wa kipekee Tanzania ambaye unaweza ukadhani alizaliwa mapema mno na alikuwa mbele ya wakati. Kwa Kiingereza tungeweza kusema ‘Mtikila was too intelligent for Tanzania!”. Jambo kubwa la kujifunza katika maisha ya utumishi wa Mtikila ni kwamba siasa ni imani iliyojengwa katika misingi fulani. 

Ni vizuri wanasiasa wanaochipukia leo wakajikita katika imani ya misingi fulani kulikoni kuendeshwa na matukio na kwenda na upepo wa kisiasa. Lakini pia tunatambua kwamba mara kadhaa ulimi wa Mchungaji Mtikila ulikuwa mkali mno kwa kiwango ambacho hakujali sana utu wa watu wengine katika mawasilisho yake. 

Hili nalo ni jambo la kujifunza na kuzingatia kwa wanasiasa wapya hapa Tanzania, kuhusu umuhimu wa kupingana katika siasa kwa misingi ya tofauti za fikra, hoja na sera bila kuvunjiana utu. Mungu airehemu Roho ya Marehemu Mchungaji Mtikila! raiamwema.co.tz

NIKIWA kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Pugu kati ya mwaka 1992 na1994, nilikuwa miongoni mwa wanafunzi ambao kila Jumamosi ilikuwa lazima twende Mnazi Mmoja, katikati ya Jiji la Dar es Salaam. Ilikuwa tunakaa huko siku nzima hadi jioni tukishindia mihogo ya kuchoma iliyokuwa inauzwa na vijana pembeni mwa barabara.


Safari yote hiyo tulikuwa tunaenda kumsikiliza Mchungaji Christopher Mtikila aliyekuwa akitoa mihadhara ya bure na katika mazingira yasiyo rasmi. Mihadhara yake ilikuwa ni mikali ikihusu Uhuru wa Tanganyika na jinsi nchi yetu ilivyokuwa ikiporwa na watu aliowaita magabachori. 


Alieleza kwa ufasaha sana kuhusu historia ya Uhuru wa Tanganyika na jinsi nchi yetu ilivyojaliwa utajiri wa rasilimali nyingi ambazo kama isingekuwa magabacholi nchi yetu ingekuwa paradiso. Kwa uzito wa hoja zake na umahiri wa kuzielezea ilikuwa ni vigumu mno kuacha kumsikiliza bila kuchoka, ama moja kwa moja au kupitia katika sauti iliyorekodiwa katika kaseti. 

Alikuwa na mvuto na nguvu kubwa ya kuongea bila kuchoka. Tungeweza kukaa Mnazi Mmoja tukimsikiliza tangu saa tano asubuhi hadi saa kumi jioni na kurudi zetu shuleni Pugu.
Baada ya Mnazi Mmoja tulihamia Jangwani ambapo Mtikila alikuwa akijaza watu wakisikiliza hotuba zake za saa ya ukombozi. Wakati huo ndio mwanasiasa pekee aliyekuwa na uwezo wa kuitisha maandamano na vijana wakamfuata Jangwani. 


Tulilundikana na tukaandamana mitaa ya Jangwani tukielekea Mnazi Mmoja bila kujua hasa tunaenda wapi hadi tulipotawanywa kwa mabomu ya machozi ya polisi. Tungesambaratika na sisi wanafunzi tungerudi zetu shuleni, na jioni nzima hiyo tungekaa kujadiliana hoja za Mtikila. Alitujaza upepo vizuri sana na tukaamini kabisa kwamba matatizo ya nchi hii ilikuwa ni hao magabachori. 

Nakumbuka katika mkutano mmoja Jangwani alijenga hoja na akawatia watu hasira dhidi ya magabachori. Tukiwa hapo, ndege ilipita angani na kwa hasira watu walianza kurusha mawe kuelekea angani wakiamini kwamba ndege hiyo ilikuwa imewabeba magabachori!

Nilipojiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1995 niliendelea kumfuatilia Mchungaji Mtikila. Wakati huo alikuwa akija pia kutoa mihadhara katika ukumbi maarufu wa Nkrumah. Kama kawaida yake, alikuwa anajaza ukumbi, siku aliyokuja chuoni wanafunzi wasingefanya chochote zaidi ya kumsikiliza. 


Kabla ya Augustine Mrema kuhamia NCCR-Mageuzi mwaka 1994/1995, Mtikila ndiye aliyekuwa mwanasiasa machachari wa upinzani aliyekuwa na uwezo wa kuitisha maandamano wakati wowote na watu wakamfuata. 

Umaarufu wake uliyumba baada ya kuanza kumpinga Mrema, wakati huo Mrema akiwa lulu na mtu yeyote aliyempinga Mrema alionekana ametumwa au kununuliwa na CCM. 

Hali hii tunaiona tena mwaka huu, na hivi karibuni kabla ya kifo chake Mtikila aliingia matatizoni kwa kumpinga vikali mwanasiasa ‘lulu’ kwa sasa na ambaye baadhi ya vyama vya upinzani vimewaaminisha wananchi kwamba ndiyo mwarobani wa mabadiliko na matatizo yote hapa nchini.

Namkumbuka pia Mchungaji Mtikila kama mwanasiasa pekee aliyekuwa na ujasiri wa kumkosoa Nyerere waziwazi bila woga na watu wakamsikiliza.


Aprili 28, mwaka 1998 nikiwa Rais wa Chama cha Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) niliitisha maandamano ya wanafunzi kuelekea Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu. Maandamano hayo, pamoja na mengine, yalikuwa na lengo la kuishinikiza serikali iongeze bajeti ya elimu. 


Hata hivyo maandamano hayo hayakufika mwisho kwani yalisambaratishwa kwa mabomu ya machozi Ubungo. Siku mbili baada ya maandamano hayo, Mchungaji Mtikila aliniita nyumbani kwake wakati huo akiwa anakaa katika ‘flats’ za NHC maeneo ya Kariako, karibu na Kiwanda cha TBL. Niliwakuta akiwa yeye na mke wake. Aliniambia kuwa “wana mpango wa kukufukuza chuo kwa sababu ya kuitisha mgomo wa wanafunzi. 

Lakini usiwe na wasiwasi tumeshakutafutia chuo huko Zimbabwe. Kwa hiyo endelea na harakati za ukombozi”. Sikutilia maanani maneno ya Mchungaji Mtikila na nilirudi zangu chuoni nikaendelea na shughuli za masomo na urais wangu wa DARUSO.

Hata hivyo, Mei 13 mwaka huo wa 1998 nilipokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu. 


Barua hiyo ilinitaarifu nia ya serikali ya kunifutia udhamini wa masomo yangu kwa kuitisha mgomo wa wanafunzi. Ndipo nikakumbuka maneno ya Mtikila. 

Niliijibu barua hiyo na nikatoa taarifa kwa wanafunzi na baada ya hapo hakuna kilichofuata hadi nilipomaliza masomo yangu mwaka 1999.

Nilitambua kwamba Mchungaji Mtikila alikuwa na taarifa za ndani sana hadi hata akajua kwamba ningefukuzwa chuo kabla ya taarifa hizo kunifikia rasmi. 


Lakini pia katika mazungumzo yake ni mtu ambaye alikuwa na taarifa za ndani mno za Tanzania na dunia kwa ujumla na ilikuwa ni vigumu kujua chanzo chake cha taarifa, hasa ukizingatia kwamba ilikuwa ni vigumu kujua kiwango rasmi cha elimu ya mwanasiasa huyu.

Nimeendelea kumfuatilia Mchungaji Mtikila katika harakati zake nyingi. 


Ni mwanasiasa ambaye amekuwa akipanda na kushuka na kupanda tena katika ulingo wa kisiasa nchini, lakini ni mwanasiasa ambaye alikataa kabisa kupotea katika ulingo wa siasa hadi mauti inamkuta.

Binafsi nitamkumbuka Mtikila kwa mambo makubwa matatu. Mosi, ni uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja na umahiri wa lugha za Kiswahili na Kiingereza. 


Nakumbuka mwaka 1998 alipokuja Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanafunzi walitaka azungumze kwa Kiingereza wakiamini kwamba haimudu hiyo lugha, na wakati huo Kiingereza mlimani kilikuwa kinathaminiwa sana kama sio kuabudiwa. Mtikila aliongea kwa Kiingereza fasaha mno hadi wote tukabaki midomo wazi.

Pili, Mtikila alikuwa ni mwanasiasa aliyeamini katika kusema kweli bila kujali ukweli huo ungemuudhi au kumfurahisha nani. Kwa kifupi yeye alikataa kuwa mnafiki. Jambo hili lilimuingiza matatizoni mara kwa mara kutokana na mazingira yetu ya siasa ambapo uwongo, ulaghai na ubabaishaji katika siasa ni sifa ya kuwa mwanasiasa. 


Tatu, ambalo linaendana na hili la pili, ni kwamba Mtikila alikuwa king’ang’anizi wa misingi aliyoaiamni. Kwa mfano, yeye tangu mwanzo kabisa wa harakati za kudai mfumo wa vyama vingi aliamini kuwepo kwa Katiba Mpya itakayotambua na kurejesha hadhi ya Tanganyika kama nchi. 

Wanasiasa wengi wamekuwa wakiyumba katika hili jambo la katiba mpya lakini yeye alibaki na msimamo huo hadi anafariki. Yeye aliamini mapema kabisa uwepo wa mgombea binafsi hadi akapigania haki hiyo mahakamani. 

Mtikila alishinda kesi kuhusu haki ya mgombea binafsi mara tatu, mbili katika Mahakama za Tanzania mwaka 1993 na 2005, na moja katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu mwaka 2010.

Mambo haya matatu yanamfanya Mtikila kuwa mwanasiasa wa kipekee Tanzania ambaye unaweza ukadhani alizaliwa mapema mno na alikuwa mbele ya wakati. Kwa Kiingereza tungeweza kusema ‘Mtikila was too intelligent for Tanzania!”.


Jambo kubwa la kujifunza katika maisha ya utumishi wa Mtikila ni kwamba siasa ni imani iliyojengwa katika misingi fulani. Ni vizuri wanasiasa wanaochipukia leo wakajikita katika imani ya misingi fulani kulikoni kuendeshwa na matukio na kwenda na upepo wa kisiasa. 


Lakini pia tunatambua kwamba mara kadhaa ulimi wa Mchungaji Mtikila ulikuwa mkali mno kwa kiwango ambacho hakujali sana utu wa watu wengine katika mawasilisho yake. Hili nalo ni jambo la kujifunza na kuzingatia kwa wanasiasa wapya hapa Tanzania, kuhusu umuhimu wa kupingana katika siasa kwa misingi ya tofauti za fikra, hoja na sera bila kuvunjiana utu.

Mungu airehemu Roho ya Marehemu Mchungaji Mtikila! - See more at: http://www.raiamwema.co.tz/pengine-mchungaji-christopher-mtikila-aliwahi-mno-kuzaliwa-tanzania#sthash.RvDk9CaX.dpuf
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: