BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ALIYEZUSHA TAARIFA ZA UONGO DHIDI YA RAIS AWAMU YA TATU KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KUKIONA CHA MOTO, MKAPA KUIBUKIA KUAPISHWA KWA RAIS MPYA TZ DK MAGUFULI DAR ES SALAAM.

Rais mstaafu Benjamin Mkapa, leo atakuwa miongoni mwa Marais wastaafu watakaoshiriki sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule, Dk. John Magufuli.
 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene, aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. 
 
Taarifa za Mkapa kuhudhuria sherehe hizo zimekuja ikiwa ni siku chache baada ya taarifa za uzushi kuhusu afya yake kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
 
Mwambene alisema serikali inalaani kwa nguvu zote taarifa hizo na kueleza kuwa uvumi huo ulienezwa kwa lengo la chuki.
Alisema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya aliyetoa taarifa hizo za uongo na za kuupotosha umma.
 
“Rais mstaafu Mkapa haumwi hata mafua, bali ni kati ya waalikwa kwenye sherehe za kumuapisha Rais Mteule Dk. Magufuli,” alisisitiza Mwambene.
 
Alisema hakuna sababu za msingi zitakazomfanya Mkapa ajitokeze hadharani ili akanushe taarifa hizo, bali kupitia  Msemaji wake, serikali ndiyo yenye wajibu.
 
Mwambene aliongeza kuwa kuhudhuria sherehe ni matakwa ya mtu binafsi, lakini  Mkapa ni miongoni mwa waalikwa.
Aidha,  alisema katika sherehe hizo za kuapishwa kwa Dk. Mgaufuli zitazofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo, Marais 15 wanatarajiwa kuhudhuria.
  
CHANZO: NIPASHE

Rais mstaafu Benjamin Mkapa, leo atakuwa miongoni mwa Marais wastaafu watakaoshiriki sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule, Dk. John Magufuli.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene, aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

Taarifa za Mkapa kuhudhuria sherehe hizo zimekuja ikiwa ni siku chache baada ya taarifa za uzushi kuhusu afya yake kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mwambene alisema serikali inalaani kwa nguvu zote taarifa hizo na kueleza kuwa uvumi huo ulienezwa kwa lengo la chuki.
Alisema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya aliyetoa taarifa hizo za uongo na za kuupotosha umma.

“Rais mstaafu Mkapa haumwi hata mafua, bali ni kati ya waalikwa kwenye sherehe za kumuapisha Rais Mteule Dk. Magufuli,” alisisitiza Mwambene.

Alisema hakuna sababu za msingi zitakazomfanya Mkapa ajitokeze hadharani ili akanushe taarifa hizo, bali kupitia Msemaji wake, serikali ndiyo yenye wajibu.

Mwambene aliongeza kuwa kuhudhuria sherehe ni matakwa ya mtu binafsi, lakini Mkapa ni miongoni mwa waalikwa. 

Aidha, alisema katika sherehe hizo za kuapishwa kwa Dk. Mgaufuli zitazofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo, Marais 15 wanatarajiwa kuhudhuria. CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: