Diwani mteule wa kata ya Sabasaba, Mudhihiri Shoo akiwa na hati ya kuchaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo sambamba na wapambe wake kufuatia kushinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu kupitia CCM katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi ya kata hiyo Manispaa ya Morogoro.
Kata hiyo ilikuwa ikishirikiwa na Naibu Meya Manispaa ya Morogoro, Mohamed Lukwele ambaye alikuwa diwani aliyemaliza muda wake lakini akang'olewa baada ya kushindwa katika kura ya maoni ya ndani ya CCM kisha kuwashinda wapinzani wa vyama vya upinzani.
MTANDA BLOG imeandaa matukio mbalimbali ya harakati za Diwani huyo mteule hatua kwa hatua na kukamilisha ndoto, hapo kuna somo kubwa kwa wanasiasa ama unapotaka uongozi ndani ya jamii, usikurupuke na kuvamia kuomba uongozi.
Msimamizi wa uchaguzi kata ya Sabasaba, Bether Kahuka kulia akimkabidhi, Mudhihiri Shoo hati ya kuchaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo huku mkewe Maua Pongwa akishuhudia.
SEPTEMBA 25/2015.
Katibu Mwenezi na Itikadi na Siasa CCM, Nape Nnaupe akimwangalia mgombea udiwani kata ya Sabasaba, Mudhihiri Shoo wakati kundi la wasanii la kuhamasisha kumpigia kura mgombea urais kupitia chama hicho Dk John Magufuli na nafasi ya ubunge na udiwani uwanja wa Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.
AUG 21/ 2015:
Afisa Mtendaji kata ya Sabasaba, Bether Kahuka kulia akikagua fomu za uteuzi za mgombea udiwani kupitia CCM, Mudhihil Shoo kushoto wakati wa zoezi za kurejeshaji fomu hizo mtaa wa Polisi Kota Manispaa ya Morogoro ikiwa sehemu ya kutimiza sifa za kugombea udiwani katika uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu, wa pili kutoka ni Katibu wa chama hicho kata hiyo (CCM), Charles Tunge na Katibu Mwenezi wake wa Itikadi na Siasa kata hiyo, Bashir Kikoro.
Afisa Mtendaji kata ya Sabasaba, Bether Kahuka kulia akipokea fomu za uteuzi za mgombea udiwani kupitia CCM, Mudhihiri Shoo kushoto ikiwa sehemu ya kutimiza sifa za kugombea udiwani katika uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu, katikati ni Katibu wa chama hicho kata hiyo ya Sabasaba, Charles Tunge.
JULAI 26/ 2015.
Mgombea udiwani kata ya Sabasaba, Mudhihil Shoo akijinadi mbele ya wapiga kura wakati wa kampeni ya kuomba kura za maoni kwa watia nia mbalimbali katika nafasi ya udiwani kupitia CCM ili kumpata mgombea moja atayepeperusha bendera katika uchaguzi mkuu ujao wa Oktoba 25 mwaka huu iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kata hiyo Morogoro.
JULAI 15/2015:Katibu wa chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Sbasaba Manispaa ya Morogoro, Charles Tunge akimkabidhi fomu Mwenyekiti wa kata katika chama hicho, Mudhihil Shoo kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya udiwani kata hiyo katika ofisi za kata ya Sabasaba, baada ya panzia la uchukuaji wa fomu za udiwani kuanza rasmi.
JULAI 15/2015:
Mwenyekiti wa kata ya Sabasaba Manispaa ya Morogoro, Mudhihiri Shoo akionyesha fomu za kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya udiwani kata hiyo katika ofisi za kata ya Sabasaba na wapambe wake.
DESEMBA 12/2014.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kata ya Sabasaba, Mudhihil Shoo wa pili kutoka kushoto akiwaongoza wanachama na viongozi mbalimbali wa chama hicho katika maandamano kutoka ofisi za kata hiyo hadi kweenye uwanja wa mtaa wa Konga kwa ajili ya kufanya kampeni ya mwisho ya uchaguzi wa serikali za mitaa katika Manispaa ya Morogoro.
OKTOBA 24/ 2014.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Morogoro mjini, Fikiri Juma kulia akimkabidhi kadi ya ya CCM aliyekuwa Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Konga kwa tikiti ya chama cha wananchi (CUF) Hamis Simba katika hafla iliyofanyika ofisi za kata CCM Kingo Manispaa ya Morogoro, katikati ni Mwenyekiti wa CCM kata hiyo. Mudhihiri Shoo.
Mwenyekiti wa CCM kata ya Sabasaba Manispaa ya Morogoro, Mudhihiri Shoo akizungumza jambo katika mkutano wa utekelezaji wa ilani ya ccm ya mwaka 2010 wakati wa hitimisho la ziara ya kuimarisha uhai wa chama kwa kata zote za Manispaa hiyo na kufanyika uwanja wa Zimamoto mkoani Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG
0 comments:
Post a Comment