BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DEVOTHA MINJA AFICHUA SIRI YA NAMNA ALIVYOSHIRIKI MAPAMBANO YA UPINZANI HUKU AKIWA MWANDISHI WA HABARI WA ITV MOROGORO.


DEVOTHA MINJA.


Mwanza. Nikiwa katika harakati za huku na kule za kuhabarisha umma, kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo nilikutana na mwanataluma wenzangu, Devotha Minja ambaye amekuwa kwenye taaluma ya uandishi wa habari kwa muda mrefu.

Devotha kwa sasa ni Mbunge wa Viti Maalum wa Maendeleo Chadema Mkoa wa Morogoro.

Katika mazungumzo yetu nilitaka kufahamu kama alikuwa na ndoto za kuwa mbunge kutokana na kuipenda kazi yake ya uandishi wa habari na kuifanya vizuri kwa weledi wa hali ya juu.

Devotha Minja ni nani
“Mimi ni mtoto wa tano na wa mwisho kuzaliwa katika familia ya mzee Mathew Minja, lakini ni mama wa watoto wawili.Nilizaliwa katika Kijiji cha Rauya Marangu mkoani Kilimanjaro,” anasema.

Alipata elimu yake sekondari katika Shule ya Kisomachi mkoani Kilimanjaro, na baadaye aliendelea na kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari ya Kibohehe iliopo Wilaya ya Hai mkoani humo.

“Nilijiunga na masomo ya uandishi wa habari katika ngazi ya stashahda mkoani Morogoro na baadaye nikaanza shahada kwanza katika Chuo Kikuu cha Sokoine mkoani Morogoro na baadaye ya shahada ya uzanivu ya Maendeleo Vijijini,” anasema.

Lini alingia kwenye uandishi
Devotha anasema alianza kazi ya uandishi wa habari katika kituo cha Radio Five jijini Arusha, kisha alifanya kazi katika magazeti ya Nipashe kama mwandishi wa kujitegemea na baadaye alijiunga na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) na kujikita kuandika makala mbalimbali za kijamii.

“Mbali na kufanya kazi kwenye magazeti nilifanya kazi katika kituo cha Abood Media na Shirika la Faraja Trust Fund la mjini Morogoro linaloongozwa na Dk Lucy Nkya.

Anasema mpaka anateuliwa kuwa mbunge alikuwa mwanadishi wa Kituo cha Televisheni cha ITV na Radio One kama mwakilishi wao mkoani Morogoro.

“Nimefanya kazi na ITV na Radio One kwa zaidi ya miaka 10 kama mwakilishi wa Mkoa wa Morogoro.”

Kuingia kwenye siasa
Devotha anasema ingawa kazi za uandishi wa habari alikuwa anazifanya vizuri, lakini alikuwa na mapenzi na Chadema ingawa kutokana na kazi yake ya uandishi wa habari hakupaswa kuonyesha anaegemea chama chochote cha siasa, hivyo ilimbidi kufanya kazi kwa kuandika habari zote za vyama vya siasa bila kuegemea upande wa chama hicho.

“Kwa kweli nilikuwa natamani kuona wananchi wanapata mabadiliko ya kweli kwa kupata ukweli juu ya mustakabali wa taifa lao, kupitia vyama vya siasa nilijua Chadema ndiyo chama pekee kitaweza kuwaeleza ukweli juu ya kupata ukombozi kamili wa Taifa hili,” anasema Devotha.

Kwa mujibu wa Devotha, alianza kujitolea kufanya kazi za siasa za Chadema bila kuweka mbele maslahi yoyote huku akitamani wananchi waelewe nini maana ya ukombozi wa pili wa taifa hili.

Devotha anasema ameshiriki harakati mbalimbali za siasa hususani katika kampeni hasa Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) ya Chadema, operesheni za futa CCM, ziara za Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) na harakazi za kupinga Katiba mpya ambazo zilizoasisi Ukawa.

“Nilitembea mikoa mbalimbali kueleza wananchi ukweli kuhusu Katiba mpya chini ya viongozi wa Ukawa, wakiwamo Dk Wilbrod Slaa katika mikoa ya Kanda ya Kati na mikoa ya Kanda ya Ziwa na Profesa Ibrahim Lipumba ambaye alifanyakazi katika mikoa ya Kusini na Nyanda za Juu Kusini,” anasema na kuongeza:

“Wakati wote sikukata tamaa nilitamani kuona siku moja Watanzania wanasikia sauti ya mabadiliko ya kweli kwa kupata haki sawa kwa maana ya rasilimali zilizopo zitumike kunufaisha kila mmoja na niliamini njia pekee ya kuleta haki hizi ni kupitia upinzani.”

Alifanyaje siasa na kazi
Devota anasema ilikuwa vigumu kutenga muda wake wa kufanya kazi ya siasa kwa kuwa alikuwa na majukumu ya kazi ambayo kama mwakilishi alitakiwa kuripoti matukio ya Mkoa wa Morogoro kwenye televisheni na redio, lakini pia alitamani kutenga muda wa kuandika habari za siasa.

“Kwa kweli ilikuwa ngumu, lakini sikukata tamaa nilijitahidi kuyafanya hayo yote kwa wakati mmoja na zaidi nilishiriki katika harakati za kuwajengea uwezo wanawake kujitambua na kutokukubali kuburuzwa... katika siasa nilikuwa nikiandaa makongamano mbalimbali ya kuwajengea uwezo wanawake,” anasema Devotha.

Atawasaidiaje wanawake?
“Nimejipanga kuhakikisha nafasi niliyoipata katika siasa ya kuwa mbunge naitumia vizuri kwani sikuipata kwa kubahatisha, naamini nina kazi kubwa mbele yangu kuhakikisha napambana ili haki za wanawake na watoto zipatikane.”

Devotha anatoa ushuhuda wa ukandamizwaji katika jamii hasa wanawake kwa kukosa sauti ikiwamo kunyang’anywa shahada zao za kupiga kura na waume zao kisha kuziuza na kupata fedha na kuwakosesha haki ya kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka.

Changamoto
Devotha anasema kwa muda mfupi alipoingia kwenye siasa amebaini vita vikubwa kila kona vya kujaribu kumvunja moyo au kumrudisha nyuma, lakini anaona hana sababu ya kukata tamaa, kwani maisha ya siasa ndiyo aliyoyaamua kuishi kwa sasa.

“Mungu ndiye atakayenipigania kwa njia yoyote ile, kwani maandiko yanasema kwani akinilinda maadui wanaonizunguka wanafanya kazi bure kwakuwa yeye hashindwi, anasema na kuongeza kuwa: “Kwenye kazi yangu ya uandishi wa habari kuna changamoto naikumbuka, nimepata misukosuko mikubwa.”

Devotha anasema anakumbuka siku aliyoandika makala ya ripoti ya migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo ilikuwa inajirudia mara kwa mara.


 “Watu walichinjana na wakulima kufunga barabara kuu ya Morogoro Dodoma lakini cha kushangaza niliitwa a na Kamati ya Ulinzi na Usalama yaMkoa Morogoro na kuniambia nasababisha mkoa huo usikalike kwa kutoa makala za vurugu, ” anasema.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: