BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWANDISHI WA HABARI AAMBULIA KURA 1 UCHAGUZI WA NAIBU MEYA MOROGORO.

Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood kulia akishuhudia naibu Meya Milikiel Mahiku na Mstahiki Meya, Paschal Kihanga (katikati) wote kutoka CCM baada ya kushinda nafasi hizo wakati wa kikao cha kwanza cha baraza la madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro juzi mkoani Morogoro. 

Na Juma Mtanda/MTANDA BLOG.
Chama cha mapinduzi (CCM) kupitia kwa wagombea, Paschal Kihanga na Milikiel Mahiku wameibuka washindi katika kinyang’anyiro cha kusaka Meya na naibu wake dhidi wa wagombea wa Chadema katika uchaguzi kumpata mstahiki meya na naibu wake wa halmashauri ya Manispaa ya Morogoro jana.

Mchakato wa kuwapata viongozi hao uliendeshwa na Katibu Tawala wilaya ya Morogoro Alfred Shao na matokeo ya uchaguzi huo kutangwa na mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Morogoro mkoani hapa.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Theresia Mahongo aliwatangaza wagombea wa CCM, Paschal Kihanga kuwa Meya wa Halmashauri ya Manispaa kwa kupata kura 36 dhidi ya Mabula Lusewe wa Cahdema aliyepata kura nne.
Mbunge wa jimbo la Morogoro, Abdulaziz Abood akitumbukiza kura katika sanduku wakati wa upigaji kura wa kumsaka Mstahiki Meya na naibu.

Mahongo alimtangaja Milikiel Mahiku wa CCM aliyemshindi mpinzani wake  wa Cahdema Juma Temba kwa kupata kura 36 dhidi ya kura nne.

 Awali katika uchaguzi wa ndani wa vyama hivyo vya kumsaka mgombea wa kuwakilisha vyama husika, CCM walijitokeza wagombea wagombea watatu katika nafasi ya umeya ambapo Paschal Kihanga aliweza kuwashinda wapinzani wawili akiwemo Meya aliyemaliza muda wake, Amir Juma Nondo.Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Paschal Kihanga wa pili kutoka kulia na diwani wa kata ya Sabasaba, Mudhihiri Shoo wa kwanza kulia wakiapa kutumikia nafasi hizo sambamba na wenzao wakati wa kikao cha kwanza cha baraza la madiwani Manispaa ya Morogoro.

Katika uchaguzi huo wa ndani ya CCM, Kihanga aliweza kumwangusha Nondo aliyepata kura 17 dhidi ya kura 20 za mshindi huku mgombea Ally Kalungwana akiambulia kura 0 na katika nafasi ya Naibu Meya, Milikiel Mahiku aliibuka kidedea mbele ya wagombe wawili.

Mahiku aliweza kupata kuwa 20 mbele ya Wenslaus Kalogeris akipata kura 16 wakati Latifa Ganzel aliyeingia kwenye siasa katika katika tasnia ya habari kampuni ya Uhuru na Mzalendo kualifanikiwa kupata kura moja.

Kwa upande wa Chadema katika uchaguzi wa ndani, nafasi ya umeya Mabula Lusewe alipendekezwa kwa kupata kura nne huku Juma Tembo naye akipendekezwa kwa kupigiwa kura nne.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: