MVOMERO SIO SHWARI: MMOJA AFARIKI DUNIA WAKATI NG'OMBE 79 WAMEKUFA KATIKA MGOGORO WA ARDHI WA WAKULIMA NA WAFUGAJI KIJIJI CHA DIHINDA MOROGORO.
Morogoro. Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba ameiagiza kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Mvomero kuimarisha ulinzi maeneo yote yenye migogoro kufuatia kutokea mapigano kati ya wakulima na wafugaji na kuua mtu mmoja na kujeruhi wengine kadhaa.
Waziri Nchemba ametoa agizo hilo leo baada ya kutembelea eneo ambapo yalizuka mapigano hayo Jumamosi Desemba 12/2015 katika kijiji cha Dihinda kata ya Kanga wilayani Mvomero.
Pia Nchemba ameagiza vyombo vya usalama kuhakikisha waliosababisha maafa hayo wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sharia
"Natoa rai kwa Wananchi hususani wa jamii ya Wafugaji na Wakulima, Hakuna ardhi au Mnyama mwenye thamani sawa na Maisha ya Mwanadamu yeyote yule,njia bora na salama ya kutatua migogoro hii inayohusisha wakuliama na wafugaji ni kufuata taratibu za kuonana na Uongozi wa serikali wa eneo husika hatua kwa hatua, ilisema taarifa ya Nchemba nakuongeza kuwa
‘’Nawaomba wananchi waache kujichukulia sheria mikononi, Tunakwenda kuunda kamati za usuluhishi wa migogoro hii kwa kila kijiji zitakazohusisha pande zote mbili ili kubaini wavamizi wa maeneo na kuwachukulia hatua za kisheria." Imesema taarifa ya Waziri Mwigulu
Licha ya mapigano hayo kuua mtu mmoja na kujeruhi wengine, pia yamesababisha hasara kubwa ambapo ng’ombe 79 wameuawa kwa kukatwa mapanga na wengine 72 wamejeruhiwa.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment