BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS DK MAGUFULI ATII AGIZO LA MKUU WA MKOA, SILAHA ZAKE ZAKAGULIWA NA ASKARI POLISI DAR ES SALAAM.



Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ametoa bunduki zake mbili aina ya shortgun na pistol na zikahakikiwa nyumbani kwake ikulu jijini Dar es salaam.

Kiongozi huyo ndiye mtu wa kwanza kutekeleza agizo la mkuu wa mkoa wa Dar es salaam la kuhakiki silaha, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.

Uhakiki wa silaha hizo umefanywa na maafisa wa Jeshi la Polisi wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Rais Magufuli ametoa wito kwa watu wote wanaomiliki silaha nchini humo kuhakikisha zinahakikiwa.




Aidha, amelitaka jeshi la polisi kuongeza juhudi za kukabiliana na watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu ili kutokomeza kabisa vitendo hivyo.

"Ni aibu kumuona askari polisi mwenye silaha ananyang'anywa silaha, ni aibu, na nasema hiyo ni aibu, mpaka jambazi akunyang'anye silaha na wewe una silaha?" amesema Dkt Magufuli.


Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: