BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHAMA CHA SIASA CHAMNG'ANG'ANIA RAIS WA NCHI ILI AONDEKE MADARAKANI.

Chama cha Democtratic Alliance nchini Afrika Kusini kumeanzisha kampeni ya kumuondoa rais Jacob Zuma madarakani baada ya mahakama ya kikatiba kutoa uamuzi kuwa alikiuka katiba.

Mahakama ilipata kuwa bwana Zuma alikataa kutii agizo kutoka kwa ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu mwaka 2014 la kamtaka alipe pesa zilizotumika kuifanyia ukarabati nyumba yake ya kibinafsi.

Vyama viwili vya upinzani viliwasilisha kesi hiyo mahakamani ili kumlazimu rais Jacob Zuma kuzingatia matokeo ya uchunguzi yaliofanywa na mkaguzi wa hesabu za serikali, kwamba alihusika na mabadiliko yaliofanyiwa nyumba yake ya Nkandla.

Mamilioni ya madola yalitumika katika kile kilitajwa na serikali kuwa uimarishaji wa usalama. Marekebisho hayo yalishirikisha ukumbi,kidimbwi cha kuogelea na zizi la ngombe.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: