BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MANENO YA KUMTAKA MKUU WA MAJESHI KUPINDUA NCHI YAMUWEKA MATATANI MWANACHUO MWAKA WA TATU TENGERU ARUSHA.

 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyage


Na Woinde Shizza, Arusha
Jeshi la polisi mkoani hapa linamshikilia mwanafunzi wa Mwaka wa tatu wa chuo cha maendeleo ya jamii cha Tengeru, Harold Mmbando (23) mkazi wa Arusha kwa kosa la kutoa taarifa za uchochezi dhidi ya Rais wa Zanzibar Dkt, Ali Mohamed Shein na Mkuu wa majeshi, Davis Mwamunyange.


Kijana huyo anadaiwa kusambaza ujumbe wa maneno makali juu ya viongozi hao.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 17 mwaka huu majira ya saa 09:00 asubuhi.

Mkumbo alisema kuwa mwanafunzi huyo alitoa taarifa za uchochezi kuhusu mkuu wa majeshi ambapo alimtaka mkuu huyo wa majeshi kupindua nchi na kusema kuwa haiwezekani viongozi wote wawe nje ya nchi huku hakuna kiongozi aliyepewa mamlaka ya kukikaimu kiti.

“Mtuhumiwa aliandika maneno kuwa Mwamunyange pindua nchi haiwezekani wote wawe nje halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya kukalia kile kiti, hayo ndio maneno aliyoyasema mtumiwa huyo “alisema Mkumbo.

Mkumbo alieza kuwa kijana huyo mbali na maneno hayo alisambaza ujumbe mwingine wenye maneno yafuatayo,” Dr Shein akiuawa kama Karume sitashangaa wala kustuka naomba mungu mauaji ya kisiasa yaliyotokea Zanzibar yawe kwa viongozi wa kisasa hasa watawala na sio wananchi wa kawaida” hayo ndio maneno aliyoyaandika mtuhumiwa huyo kupitia mitandao ya kijamii kama faccebook.

Mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapo kamilika huku akitoa rai kwa watu wote wanaotumia mitandao ya kijamii kutumia mitandao hiyo ya kijamii pasipo kukiuka sheria na taratibu za kisheria.


Alitumia muda huo pia kutoa onyo kali kwa yoyote atakaye bainika anatumia mitandao vibaya na kusema kuwa atachukuliwa hatua kali za kisheria dhidi yake. 

Wakati hayo yakiendelea mshtakiwa wa kesi ya kumtukana Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli Isaac Emily (40), mkazi wa Olasiti jiji hapa inatarajiwa kuanza kusikilizwa mfululizo kuanzia Juni 5 mwaka huu katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: