Morogoro. Serikali imeombwa kufunga mtambo wa kuchunguza na kufuatilia makosa ya mtandaoni badala ya kwenda kwenye kampuni za simu kukusanya ushahidi.
Ombi hilo lilitolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei huku akitaja makosa yanayofanywa kwa njia ya mtandao kuwa ni ujambazi, wizi wa fedha benki, udhalilishaji na lugha za matusi.
Alisema endapo kutakuwa na mtambo wa kufuatilia makosa hayo, polisi itakabiliana na matukio hayo haraka.
Alionya kuwa Sheria ya Mitandao ipo na haitamuacha mtu atakayefanya uhalifu huo.
Kamanda Matei alitoa rai kwa wananchi hususani vijana kuwa makini na makosa hayo ili kuepuka kutiwa hatiani kwa sababu wapo wanaohukumiwa kwa kufanya makosa hayo bila kujua.
Mapema wiki hii, watu 12 walifikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumbaka mwanamke mmoja mkazi wa Morogoro, Dakawa, kisha kumrekodi na baadaye kusambaza picha za video zinazoonyesha wakifanya kitendo hicho cha kinyama na udhalilishaji.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment