Katika mashtaka wanayokabiliana nayo ni pamoja na kumbaka msichana huyo, kumpiga picha za utupu za video na kuzisambaza katika mitandao ya kijamii, katika nyumba ya kulala wageni ya Titii iliyopo Dakawa wilayani Mvomero.
Watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani leo na wengi wanne kati ya 11 wakiwemo waliopokea picha hizi za video na kusambaza video.
Wengine wanaotuhumiwa kusambaza picha hizo za utupu za video ni pamoja na Rajabu Salehe (26), Saidi Athmani (26), Musini Ngai (36) Saidi Mohamedi (24), John Peter (24), Hassan Ramadhan (27), Ramadhan Ally (27), Musini Ngahyi na Ramadhan Ngonja.
Watuhumiwa walinyimwa dhamana na kupelekwa mahabusu ya magereza ya mkoa kwa kile kilichoelezwa na waendesha mashtaka wa serikali kuwa watavuruga ushahidi ambapo watuhumiwa hao watafikishwa tena Juni Mosi mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment