Bondia Mohamed Ali kushoto akimshambulia mpinzani wake kwa makonde mazito.
Bondia wa zamani wa Marekani, Mohamed Ali ambaye alikuwa ni miongoni mwa watu maarufu na wenye wapenzi wengi duniani, amefariki akiwa na umri wa miaka 74 kutokana na tatizo mfumo wa kupumua.
Bingwa huyo wa dunia katika uzani wa juu wa zamani alilazwa katika hospitali siku ya alhamisi June 02 mwaka huu kufuatia tatizo lililojitokeza katika mapafu.Mohamed Ali mbali na kupatwa na tatizo hilo alikuwa akiugua kiharusi na alipatikana na ugonjwa wa Parkinson mwaka wa 1984 baada ya kustaafu ngumi za kulipwa .
0 comments:
Post a Comment