Bukombe. Mkuu wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Amani Mwenegoha ameagiza kufutwa kwa sheria kandamizi ya kuwatoza wafugaji kiasi cha Sh50, 000 kwa kila ng’ombe inayoingia shambani kwa mtu na kulisha mazao.
Akizungumza kwenye mkutano wa wafugaji juzi, Mwenegoha alisema sheria zilizowekwa na serikali za vijiji viondolewe, pia wafugaji wasiingize ng’ombe zao kwenye pori la akiba.
“Sheria mliyoiweka inawakandamiza wafugaji, pia fedha zinazotolewa baada ya kukamatwa hazionekani kufanya kazi yoyote, hivyo iondoeni kwa sharti la kutoingiza ng’ombe zao kwenye pori la akiba,” alisema Mwenegoha.
Mmoja wa wafugaji waliohudhuria kikao hicho, Mashaka Shabani alisema kutokana na wingi wa ng’ombe wao wamekuwa wakitozwa faini kubwa kwa kila ng’ombe atakayeonekana ameingia shambani.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment