BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KIPINDUPINDU CHAWAFUKUZISHA TIMU YA MUHEZA UNITED FC LIGI YA MABINGWA WA MIKOA MOROGORO.


Juma Mtanda, Morogoro.
Timu ya soka ya Muheza United FC ya mkoani Tanga imejitoa kuendelea kushiriki ligi ya mabingwa wa mikoa baada ya wachezaji 10 na daktari mmoja kukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu Mei 29 mwaka huu katika ligi inayoendelea kwenye kituo cha Morogoro.

Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, Msimamizi wa kituo cha ligi ya mabingwa wa mikoa Morogoro, Charles Ndagala amethibitisha kupokea barua ya kujitoa kwa timu ya soka ya Muheza United FC ya Tanga kutokana na sababu za kiafya zilizowakumbwa wachezaji wao.

Ndagala alisema kuwa katika barua hiyo iliyoandikwa na Katibu mkuu wa timu ya Muheza United FC imewasirisha sababu za kujitoa kwa timu kushindwa kumalizia michezo miwili kutokana na matatizo ya kiafya yaliyotokana na sehemu kubwa ya wachezaji kukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu.

“Tumepokea barua ya timu ya Muheza United FC ya kushindwa kwao kutomalizia mechi mbili zilizobakia kutokana na afya za wachezaji nah ii timu Mei 29 mwaka huu baadhi ya wachezaji wake wameugua ugonjwa wa kipindupindu.”alisema Ndagala.

Katika barua hiyo (Nakala tunayo) imeeleza kuwa timu ya Muheza United FC mei 29 mwaka huu usiku walipatwa na matatizo ya kuuguliwa na wachezaji wao pamoja na daktari kuugua ugonjwa wa kipindupindu.

“Wachezaji wangu 10 na daktari wa timu mmoja kufanya kufikia idadi ya watu 11, hivyo wachezaji waliobakia walikuwa 13 kupatiwa kinga ya vidonge na baada ya kutolewa hospitalini baadhi ya wachezaji walicheza na timu ya Stend Misuna FC Juni mosi baadhi walishindwa kumaliza mchezo”ilisema taarifa hiyo.

Ilisomeka taarifa hiyo na kufafanua kuwa baada ya mchezo kumalizika na wachezaji kurudi kambini hali ilikuwa mbaya huku mwalimu wa timu hiyo, John Kibwana hawezi kuwa na maamuzi kuwachezesha wachezaji wanaoumwa.

Akizungumzia hali hiyo kocha huyo, alisema kuwa tayari timu imeandika barua ya kushindwa kumalizia kutokana na hali za wachezaji kutokuwa mzuri na imani yao ombi lao litakubaliwa kwani mchezo ni afya na pasipo na afya hakuna michezo.

Timu ya Muheza United FC tayari imeshacheza michezo dhidi ya Sifa Politan FC na kumalizika kwa sare ya1-1 mei 24 wakati mei 26 ilimenyana na Makumbusho FC ya Dar es Salaam kutoka suluhu ya 0-0.

Michezo mingine Muheza United FC ilicheza na Mbuga FC ya Mtwara mei 28 na kutoka suluhu ya 0-0 huku mei 30 ilitarajiwa kucheza na Stend FC Bagamoyo lakini mchezo huo hakufanyika kutokana na wachezaji kukumbwa na pindupindu.

Juni mosi Muheza United FC ilishuka dimbani na kucheza na Stend Misuna FC ambapo mchezo huo Muheza United FC iliambulia kipigo cha bao 2-1 wakati mchezo wao wa mwisho ulitarajiwa kucheza na Namungo FC ya Ruangwa Lindi.

Namungo FC ndio inayoongoza ligi hiyo kituo cha Morogoro kwa kukusanya pointi 10 ikifuatiwa na Stend Misuna FC yenye pointi tisa huku Sifa Politan FC ya Dar es Salaam ikiwa na pointi sita.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: