BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MADEREVA WA MAGARI NA PIKIPIKI WAITAJIRISHA POLISI MOROGORO KIASI CHA SH 288 NDANI YA MWEZI TU MWAKA 2016.

Morogoro.Polisi Morogoro imefanikiwa kuingiza Sh 288 milioni kutokana na tozo mbalimbali za makosa ya usalama wa barabarani kwa kipindi cha Mei mwaka huu.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amesema jana kuwa makosa hayo yamepatikana baada ya operesheni maalumu kufanywa na jeshi hilo kuanzia Mei Mosi hadi Mei 30.

Amesema kiasi hicho cha fedha kilipatikana kutokana na jumla ya makosa 9,612 kwa magari na pikipiki katika mkoa wa Morogoro.

Alitaja makosa ya magari kuwa ni mwendo kasi makosa 2661, ubovu wa magari makosa 988, kukiuka ratiba makosa 275, kuzidisha abiria makosa 113, kutokuwa na bima makosa 114 na mengineyo 2,908.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: